December 17, 2018


Baada ya dirisha dogo la usajili kufungwa Disemba 15, imeelezwa kuwa Kocha Mkuu wa Yanga alipendekeza baadhi ya wachezaji kusajiliwa lakini mabosi wake wakafanikiwa kumnyaka Haruna Moshi pekee.

Kitendo hicho kimeonesha kumkera Zahera na kuwaambia endapo Yanga itaukosa ubingwa basi asilaumiwe.

Kocha huyo ambaye amekuwa hana unafiki tangu ajiunge na Yanga, ameeleza kuwa kuna usajili umefanyika ambao haukuwa pendekezo lake.

Moja ya usajili huo ni ule wa kipa Ibrahim Hamid ambao hakuupendekeza lakini mabosi wake wakaamua kumsajili.

Wachezaji ambao imeelezwa Zahera aliwapendekeza ni hawa hapa:-

1. Farouk Shikhalo (Bandari) 
2. Haruna Moshi Baban (African Lyon)
3. Charles Ilanfia (Mwadui FC)
4. Umar Kasumba (Sofapaka)

3 COMMENTS:

  1. Ni vema mawazo ya kocha na ushauri wake uheshimiwe kama uwezo wa kifedha unaruhusu

    ReplyDelete
  2. Sawa ninakubaliana na suala la uwezo lakini kwa nini alidanganywa kama kila kitu kiko tayari na wachezaji watapatikana uongo mwingi unajenga taswira mbaya kwenye kuendeleza vilabu vyetu ni lazima viongozi wawe wa wazi na wa kweli.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic