December 17, 2018


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema amechukiwa na mabosi wake kufanya usajili wa golikipa Ibrahim Hamid ambaye hakuwa pendekezo lake.

Zahera ambaye aliiongoza Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu Bara jana, alisema hayo ikiwa ni baada ya mechi hiyo kumalizika.

Zahera alieleza kuwa mabosi wake wameamua kumzunguka tofauti na maagizo ambayo aliwapa ili kufanya usajili.

Kitendo hicho kimefanya Zahera ashindwe kuvumilia na kuamua kuwachana LIVE viongozi wake bila ya kuonesha hofu ya kufuzwa kazi.

Aidha, Zahera amewataka wanachama na wapenzi wa Yanga kuwa asilaumiwe endapo timu hiyo itakosa ubingwa msimu huu baada ya waajiri wake kufanya usajili ambao haukuwa pendekezo lake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic