December 25, 2018


Hii hapa orodha ya wachezaji waliofunga mabao kuanzia matatu na kuendelea katika Ligi ya Mabingwa Afrika

1. Moataz Al-Mehdi (Al Nasr) -7
2. Clatous Chama (Simba) -4
3. Meddie Kagere (Simba) -3 
John Bocco (Simba) -3
Sikiru Alimi (Lobi Stars) -3
Jeremy Brockie (Mamelodi Sundowns) -3
Kamilou Daouda (Cotton Sport) -3
Sami Hien (ASF Bobo Dioulasso) -3
Lazarous Kambole (Zesco) -3
Bolaji Sakin (Horaya) -3
Mamadou Sidibe (Jimma Aba Jifar) -3

1 COMMENTS:

  1. Najua wachezaji wazawa wanapambana pale Simba ili kujenga uwezo wao na kumshawishi mwalimu wao awaamini na kuweza kuwapa nafasi ya kucheza ila ninachokiamini mimi bado kasi yao ya kujituma bado ni ndogo au wanakosa kujiamini.Nilimuona Mkude wakati anaingia uwanjani kwenye mechi ya Nkana na masihara yake akiiga staili ya sala au dua ya wachezaji wa Nkana. Lakini nilichokuwa nakitizama na kilichonivutia kwa Mkude sio ile ishara ya mkono wake kuzichana nywele zake kwa hewa hapana bali nilishangazwa na jinsi alivyokuwa amerilax wakati anaingia uwanjani huku akitabasamu kwa utani katika kwenda kuukabili moja ya mchezo muhimu kabisa katika maisha yake ya soka na kule ni kujiamini kwa mchezaji na si shingai kumuona Mkude akidumu katika first eleven ya Simba kwa muda mrefu na naamini kinachombeba sio kama anajua sana bali anajiamini. Kuna wachezaji kadhaa wazawa pale Simba nnaimani walishakwiva zamani sana lakini tatizo lao ni kukosa kujiamini na kumuaminisha kocha kuwa wanaweza. Wakati mwengine sio zambi kumuomba mwalimu mechi ili kuthibitisha ubora wako kama unajiamini kuliko kusubiri majaliwa. Saidi Ndemla,Mzamiru, Yasini, Adam Salamba, Shiza kichuya hata Paul Bukaba hawa vijana ni mahiri sana na wanauwezo wa hali ya juu wa kusukuma kabumbu asikwambie mtu na ni wachezji wa kuiteka Simba hivi sasa ila ninachokiamini wana tatizo la kutojiamini. Mzamiru Yasini ni mchezaji mwenye kasi na shabaha ya ajabu ya kutumbukiza mipira wavuni sasa sijui kujiamini kule kumepotelea wapi kwani baadhi ya nafasi nyingi za wazi za mabao zinazopotezwa na fowadi andamizi ya Simba hivi sasa kama zinamkuta Mzamiru au Kichuya walio kwenye ubora wao wala Simba na wanasimba kamwe wasingefikiria kutafuta fowadi. Kwani Walter Bwalya na Mzamiru wanapishana nini? Hapana, ila tofauti zao ni hali ya kujiamini mchezoni kati ya wawili hao. Bwalya miaka 23 tayari kapteni timu kubwa kama Nkana. Lakini bila ya kuongeza chumvi Mzamiru alie kwenye ubora wake na kama angekuwa anaishi na kuudumisha ubora huo basi Bwalya mbele ya Mzamiru ni cha mtoto. Sasa Simba imebahatika kuingia hatua ya makundi ni wakati muafaka kwa wachezji wa Simba kujitangaza kimataifa na kutoka au hata kama hawakutoka basi waongeze viwango vyao iwe hata akibakia Simba awe mchezaji muandamizi na ili Simba kumzuia asiondoke lazima jasho liwatoke. Ninachojaribu kuwasihi vijana kama ujumbe utafika hawana cha kuhofu pale Simba kwani hata huyo kocha kawakuta pale Simba. Wanachotakiwa kufanya sio kuwa hofu bali ni kumtia hofu ya heshima kocha wao kutokana na uwezo wao kama anavyohofu kumpoteza Emanuel Okwi asiondoke. Sasa vijana kama mlikuwa mkiwaza safari ya ulaya au kuajiriwa na moja ya vilabu vikubwa na tajiri barani Africa utaanzaje? basi hatua ya makundi ni moja ya bahati kubwa kuweza kuulizia kwa vitendo safari hiyo. Hivi karibuni nilimsikia mchezaji Nguli wa zamani wa Simba Mtemi Ramadhani akisema na nadhani hata wachazaji wenyewe wamemsikia akisema kuwa wachezaji wengi wa Simba hawapo fiti,wapo walaini mno wakiguswa na kibuyu kidogo tu chali. Ila cha kushangaza hawa vijana wetu kwanini wanashindwa kuwafuata wazee kama hawa akina Mtemi Ramadhani kupata maarifa japo kiutani kumuuliza mzee mimi nimeshajiumiza sana na wewe bado unasema nipo mlaini inakuwaje lakini? Nifanye nini sasa? Kwa sisi tunaemfahamu Mtemi Ramadhani wakati akicheza mpira alikuwa sio mchezo ni miongoni mwa mafundi hasa, kuna madini mengi ya kimaarifa kutoka kwa Mtemi Ramadhani asipuuzwe na hata na viongozi wa Simba ni moja ya hazina halisi katika klabu ya Simba iliyobakia pamoja na Kibadeni na wengineo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic