December 11, 2018


Uongozi wa kupitia kikao cha Matawi kilichoketi jana jijini Dar es Salaam kwa pamoja kimekubaliana kwenda mahakamani kufungua kesi mbili.

Kikao hicho kimeamua kufanya maamuzi hayo ambayo moja ya kesi hiyo ni kujua tafsiri sahihi ya sheria juu ya uchaguzi wao kusimamiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) badala ya wao wenyewe.

Ukiacha na uchaguzi, suala lingine ambalo Yanga limewaamua kufanya maamuzi hayo magumu ni kuwashitaki viongozi wa juu wa TFF, Rais Wallace Karia na Katibu Mkuu, Wilfre Kidao ambao hawatambui kuwa Yusuf Manji ni Mwenyekiti wa klabu yao.

Kuhusu Manji, wanachama hao wameeleza kuwa Manji anatambulika kuwa Mwenyekiti kwani katika mkutano mkuu wa mwisho uliofanyika walikubaliana kwa pamoja kuwa ndiye atakayeendelea kushikilia nafasi hiyo.

Wanachama hao watatinga mahakamani muda wowote kuanzia hivi sasa ili kupata haki yao tayari kujua hatima ya uchaguzi na juu ya suala na Manji kutotambulika kama ni Mwenyekiti wa Yanga.

2 COMMENTS:

  1. hawa wanataka Tanzania simba ifungiwe na fifa ili kuwakomoa Simba baada ya kuona wanafanya vizuri kimataifa

    ReplyDelete
  2. KAMA TFF WANAENDESHA MPIRA WA TANZANIA KWA KUFUATA SHERIA ZA FIFA HAWATOFUNGIWA NA KAMA WANATUMIA UBABE ILI MRADI KUIKOMOA YANGA ACHA TUFUNGIWE !!

    IFIKE WAKATI WATU WATAMBUE KUA MPIRA NI MCHEZO UNAOCHEZWA UWANJANI NA MATOKEO YANAPATIKANA PALE PALE UWANJANI NA SI KUTUMIA SIASA KUKANDAMIZA TIMU PINZANI

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic