MCHEZAJI YANGA AWAPELEKA MABOSI WAKE CAF, KAMA UTANI VILE KUMBE....
Aliyekuwa Mlinda mlango wa Yanga, Mcameroon Youthe Rostand, ameamua kuipeleka Yanga katika Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutokana na kushindwa kumlipa fedha zake.
Inaelezwa kuwa Rostand ameandika barua kwenda CAF kuishitaki Yanga kwa sababu za kumlipa fedha za kuvunja mkataba wake.
Kipa huyo ambaye alipojiunga na Yanga alisaini mkataba wa miaka miwili na kufanikiwa kumaliza mmoja kabla ya ule wa pili kuyeyuka kutokana na kuonesha kiwango kiwango duni dimbani.
Hivyo baada ya kuvunjiwa mkataba wake, Rosrand alikubaliana na Yanga kulipana fedha za uvunjaji wa mkataba huo lakini cha kushangaza mpaka sasa hakuna malipo yoyote yaliyofanyika.
Kipa huyo alijiunga na Yanga akitokea African Lyon ya Dar es Salaam kisha kumwaga wino wa miaka miwili na Yanga 2017.
0 COMMENTS:
Post a Comment