December 11, 2018






NA SALEH ALLY
YANGA wameongeza mchezaji mwingine raia wa DR Congo ambaye amejiunga na kikosi hicho akitokea nchini mwao.


Harakati za kukamilisha usajili wa Reuben Bomba ambaye imeelezwa anacheza kama kiungo wa pembeni kulia na kushoto lakini katikati kama namba kumi zilikuwa zinatarajia kukamilika kati ya jana na leo.


Tayari Bomba ameanza mazoezi na imeelezwa kwamba ni mmoja wa wachezaji ambao wameanza kuonyesha cheche zao mazoezini licha ya kwamba ni siku chache.


Jambo zuri, ubora wake utaonekana baada ya kuanza kucheza katika mechi za mashindano kwa kuwa mazoezi yanaweza kutoa dira ya mwelekeo wake kuwa ni mchezaji wa aina gani.


Ujio wa Bomba unaifanya Yanga kuwa na wachezaji wanne wa kigeni kutoka nchini DR Congo. Idadi inaweza kuwa tano kwa kuwa hata kocha mwenyewe ni raia wa DR Congo.


Kuna kiungo Papy Tshishimbi, kipa Claus Kindoki, mshambuliaji Herietier Makambo na sasa Bomba.


Nimeamua kueleza wazi na mapema kuhusiana na suala la idadi ya kuwa na wachezaji wa kigeni kwa wingi kutoka katika nchi moja. Hili limekuwa ni tatizo na kama unakumbuka niliwahi kulizungumza sana wakati huo Simba ina wachezaji sita kutoka nchini Uganda.

Wachezaji hao baadhi walikuwa wakiongozwa na akina Sserunkuma wawili, Juuko Murshid, Emmanuel Okwi, pamoja na Hamis Kiiza na mwisho wake Simba haikufanya vema zaidi ya kuambulia mzigo wa migogoro na wachezaji hao.

Suala la msingi kabisa huwa ni wachezaji wazuri lakini lazima kuangalia namna ya kuendesha timu itakuwaje. Suala la tahadhari ni bora zaidi katika uendeshaji kwa kuwa wachezaji wanaotokea nchi moja, wakiwa wengi wao hutengeneza himaya yao.

Kama utakuwa na wachezaji kuanzia wanne kutoka katika nchi moja, baada ya muda hawa hutengeneza himaya yao ndani ya himaya ya wenyeji na mwisho suala la kushindana nguvu kila upande ukitaka kuonyesha ukubwa wake huanza.

Mara nyingi hali kama hii inabadilika na kuwa tatizo katika afya ya kikosi hasa kama wale wachezaji wageni watafanikiwa kufanya vizuri zaidi maana watataka kuonekana ni bora zaidi kwa kuwa kunakuwa na suala la “mob psychology”.

Unajua inakuwa hivi; wakati kuna wachezaji watatu wanafanya vizuri kutoka DR Congo, huenda kama wako watano, wawili wanaweza kuwa wanaboronga. Hawa watataka kukombolewa kupitia mafanikio ya wengine na hapa njia rahisi ni kutengeneza uchonganishi kwa wengine. 

Utakuta wale wanaofanya vizuri wakawa wanatumika bila ya kujua. Mwisho ndani ya kikosi kimoja kunakuwa na makundi mawili yanayopigania ukubwa badala ya kuungana kuisaidia timu. 

Kawaida kwa kocha kama Zahera, kwake kiramani inakuwa rahisi kuchukua wachezaji nyumbani kwao. Kumbuka ni kocha wa timu ya taifa na suala la kujua wapi kuna mchezaji mzuri linakuwa ni jambo lisilo na ugumu hata kidogo. 

Tayari tumeona Kindoki amefeli, hili halina mjadala labda abadili mambo hapo mbele. Kama ni haki bin haki, lazima apunguzwe lakini lazima kuwe na mjadala ambao hauna sababu kwa kuwa kocha atajaribu kumlinda na wenzake watajaribu kutengeneza ushawishi ikiwemo kusema wanamjua ni mzuri na hajatulia.

Vema kuwe na wachezaji wa kingeni waliogawanyika kutoka katika nchi tofauti. Hapa nazungumzia ubora wa wachezaji wenyewe pamoja na afya ya endeshaji wa klabu kuhakikisha inakwenda bila ya migogoro au migongano isiyokuwa na ulazima au ile inayoepukika.

Hivyo, kama Zahera ataongeza mchezaji mwingine baada ya Bomba, awe anatokea DR Congo, itakuwa ni kuandaa mvurugano ambao unaweza kuiathiri Yanga. Mfano, Zahera akiondoka au kuondolewa (yote yanawezekana), watakaobaki pia hawatakuwa na furaha sana.

Pia inawezekana wakati ni wachezaji wazuri, Yanga inawahitaji lakini wakaondoka kiulauni au wakagoma kuongeza mkataba kwa kuwa wataitwa na lengo litakuwa ni kwenda aliko kocha. 
Vizuri sana kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni kutoka katika nchi moja. Yanga wanaweza wasilione hili sasa lakini baadaye likawa lina athari kubwa.

Niliwahi kuwaambia Simba kuhusiana na idadi kubwa ya Waganda katika kikosi chao, nilisisitiza haikuwa sahihi. Nilipokutana na kiongozi mmoja wakati ule, akaniambia ninatumika. Nilishangazwa sana.

Ajabu zaidi, baada ya idadi ya Waganda kuwa kubwa kuonekana ni tatizo kwao, siku moja tulipokutana, nilimuuliza shida ya Waganda ilikuwa ni nini. Kwa kuwa alikuwa amesahau, alinihadithia yale niliyokuwa nimeandika katika makala waliyoiponda na ajabu kabisa ambacho niligundua sisi wanadamu tumeumbwa na kusahau.

Ni pale aliponiambia yeye amekuwa na wazo la kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni kwa wingi kutoka katika nchi moja, lakini viongozi wenzake wamekuwa hawamuelewi na sasa inaonekana watakuwa wamemuelewa!

7 COMMENTS:

  1. Ndumilakuwili, nimekutoa thamani, unapenda matatizo ya Yanga maana ndio kula yako nenda katengeneze majungu kumtumia mzee Akilimali. Achana na Yanga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nikweli hapo Salehe ametahadharisha maana tuliona wakati wa Mikia wakiwa na wale wachezaji 6 toka kwa M7.

      Delete
  2. ARSENEL WENGER HAKUWAHI KUWA NA MATATIZO PALE ALIPOKUWA ANAWAJAZA WAFARANSA KIKOSI CHA ARSENAL KILA MWALIMU ANA FALSAFA YAKE MKUU

    ReplyDelete
  3. LAKINI HAYO YA YANGA HIVI WEWE MWANDISHI YANAKUHUSUJE? HUKO NI KUWAINGILIA YANGA. HATA KAMA ULITOA USHAURI KWA SIMBA BADO IBAKIE KAMA USHAURI TU KLABU ZENYEWE ZINA MAAMUZI YA MWISHO. YANGA WAKITAKA KUCHUKUA TIMU YA TAIFA YA DRC WATOKE WACHEZAJI 10 KATI YA 11 RUKSA. TATIZO LIPO WAPI? NI MAAMUZI YA KLABU ILI MRADI KANUNI ZA USAJILI ZINARUHUSU.

    ReplyDelete
  4. Sawa umeandika vizuri,kindoki si anapunguzwa kesho tu watabako watatu,lakini uliwahi kumkazia ngoma ukasema haumwi kumbe masikini anaumwa kweli hilo lilionekana wakati amekwenda Azam hadi wakakamilisha matibabau sikukuona.hapa kuja kutubu!

    ReplyDelete
  5. Sawa umeandika vizuri,kindoki si anapunguzwa kesho tu watabako watatu,lakini uliwahi kumkazia ngoma ukasema haumwi kumbe masikini anaumwa kweli hilo lilionekana wakati amekwenda Azam hadi wakakamilisha matibabau sikukuona.hapa kuja kutubu!

    ReplyDelete
  6. Salehe nilikuwa napenda Sana makala yako lkn toka umeanza kumhoji akilimali kila siku nimekushusha..Hanna gazeti lingine linalomhoji yule mzee ksbb ni mtengeneza matatizo na Hana msaada wowote kwa timu..lkn we kila siku unampa fursa kuvuruga..turudi kwa Zahera kusajili wacongo..Zahera anajua mpira kuliko ww..ni kocha msaidizi wa national team ya Congo..anavumilia matatizo yote ya Yanga na timu inafanya vizuri..mwache asajili anaoona wanafaa..usimwingilie..usijifanye unajua kuliko Hussein nyika,kaaya..Matatizo yapo na hata yakitokea yatapita tu..Viva Zahera..Viva Yanga..kaa kimya..tuachie Yanga yetu na matatizo yetu..endelea kumnadi akilimali asiye na msaada wowote kwenye mpira zaidi ya mboyoyo..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic