January 24, 2019


Soka la wanawake nchini linazidi kukuwa kwa kasi siku hadi siku ambapo wachezaji wengi wa jinsia hiyo wanaendelea kuonyesha vipaji vyao kwa sasa kupitia Ligi Kuu ya Wanawake Tanzana Bara ambayo inadhaminiwa na Serengeti Lite na kuzishirikisha timu 12.

Hadi sasa JKT Queens inaongoza ikiwa na pointi 21 baada ya kushinda mechi zake zote. Katika ushindi wao, kuna baadhi ya mechi imeibuka na mabao mengi. Wachezaji wawili wa JKT Queens mpaka sasa wanaonekana kuwa hatari katika kuzifumania nyavu kwenye ligi hiyo.

Wachezaji hao ni washambuliaji Asha Rashid ‘Mwalala’ na Fatuma Mustapha. Wawili hao peke yao mpaka sasa wamefunga jumla ya mabao 31. 

Mwalala anayo 13 akishika nafasi ya pili kwa ufungaji na Fatuma ndiye kinara akiwa nayo 18. 

“Mimi ni mtoto wa mwisho katika familia yetu ya watoto watatu. Kaka zangu wawili mmoja ndiye aliyekuwa akicheza soka. Alikuwa kwenye timu ya Toto Africans akicheza nafasi ya golikipa. Anaitwa Lusajo. 

“Nimezaliwa Mwanza, nimekulia Mwanza na nimesoma hukohuko. Baba yangu ni Mzigua wa Tanga na mama ni Muhaya.

“Nilianza kucheza soka tangu nikiwa darasa la kwanza huko Mwanza, kaka yangu alikuwa ananichukua sana kwenda uwanjani. “Wakati huo yeye alikuwa ni golikipa wa Toto, kuanzia hapo ndipo nilianza kuwa na mapenzi na soka. 

“Baada ya mama yangu kugundua kuwa nina kipaji cha kucheza soka, akaamua kuanzisha timu yake ya wasichana ili nipate nafasi ya kucheza soka na kukuza kipaji changu.

Hiyo timu ilikuwa inaitwa Mwanza Heroes. “Baada ya kucheza hapo kwa muda, nikajiunga na Marsh Queens, baadaye nikapita Mburahati Queens, mwisho wa siku ndiyo nikatua hapa JKT Queens.

USHAWAHI KUMPA ZAWADI BAADA YA KUFIKA HAPO ULIPO?

“Kusema nimewahi kumpa kitu kwa ajili ya fadhila ambazo amenifanyia itakuwa ni uongo, ninachofanya ni kila siku huwa najitahidi kumpa zawadi ambazo zitamfurahisha kwa sababu napenda kumuona akitabasamu.

KIPI KINACHOKUPA CHANGAMOTO KWENYE SOKA LA WANAWAKE?

“Kuitwa dume jike kisa tu nacheza soka, hicho kitu kinanichukiza sana na sipendi  Asha kusikia mtu akiniita hilo jina. “Utakuta mtu au shabiki amekuona u w a n j a n i unacheza soka anakuuliza kwa nini unacheza soka kwani wewe ni dume jike?

Kiukweli huwa nachukia sana mtu akiniita hivyo wakati mimi mrembo kabisa. “Pia sipendi watu wanapoipuuza Timu ya Taifa ya Wanawake, wanasahau kuwa inawakilisha taifa, niwaombe Watanzania wasitupuuze kwa sababu siyo muda mrefu tutaenda Kombe la Dunia.

MAFANIKIO YAKO KWENYE SOKA NI YAPI?

“Soka limenipa vitu vingi sana vya ndani ya uwanja na nje ya uwanja kwani limeninyanyua na kunipa mwanga mzuri wa maisha.

MBALI NA SOKA, UNAFANYA NINI?

“Mimi ni mjasiriamali na mfugaji wa kuku, bata, mbuzi na ng’ombe. Ninao wengi sana, kama kuna mtu anahitaji anaweza kunitafuta tufanye biashara.

ULISHAWAHI KUCHEZA SOKA NJE YA NCHI?

“Ndiyo, kuna kipindi niliwahi kupata timu Uturuki na nilicheza kwa miezi minne kwenye Klabu ya Atasahal ipo Instabul, lakini nilishindwa kudumu kwa kuwa nilikosa kibali cha kufanyia kazi. “Kipindi ambacho nilienda kule, Uturuki walikuwa wanapambana wajiunge kwenye Umoja wa Ulaya, hivyo ilikuwa ngumu kupata vibali vya kubaki pale.

IKITOKEA TIMU NYINGINE KUTOKA ULAYA IMEKUFUATA UPO TAYARI KWENDA?

“Kuna timu mbili zinanihitaji kwa sasa, moja ipo Afrika Kusini na nyingine Sweden, lakini ugumu ni kwamba mimi kwa sasa ni muajiriwa wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kwa hiyo zile timu zinapaswa zifuate utaratibu. 

“Naamini mabosi zangu hawawezi kunizuia kuondoka kwenda sehemu yenye manufaa makubwa kwangu, hivyo basi kama watafuata utaratibu nipo tayari
kwenda.

HASSAN KESSY ULIKUTANA NAYE WAPI?

“Nilikutana naye muda mrefu kidogo, nakumbuka wakati ule yeye yupo kwenye timu ya taifa ya vijana na mimi nilikuwa nakuja hapo kufanya mazoezi, hivyo ndivyo tulivyokutana na kuanza urafiki. “Nipo na Hassan kwa muda wa miaka mitano sasa na tunaishi wote kwenye nyumba
moja na kwetu wanamfahamu na mimi kwao wananifahamu. 

Kwa hiyo mipango ya kuanzisha familia kwa hapo baadaye basi yawezekana ikawa na yeye Hassan.

MMEPANGA KUWA NA WATOTO WANGAPI?

“Mimi binafsi yangu natamani kuwa na watoto watatu, lakini sijajua kwa upande wa Hassan yeye anataka kuwa na watoto wangapi.

KESSY NI MTU WA AINA GANI AKIWA NYUMBANI?

“Mcha Mungu, mpole, msikivu na siyo mgomvi, huwa nashangaa sana nikisikia watu wanasema kuwa Hassan ni mkorofi.

CHANZO: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. Habari inakosa mtiririko mzuri. Mwandishi amekosa focus.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic