January 20, 2019


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameamua kuuwasha moto kwa Waamuzi wa Ligi Kuu Bara baada ya kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Stand United.

Zahera ambaye timu yake ilifungwa kwa bao 1-0 huko Shinyanga ameeleza kuwa waamuzi wa soka la Tanzania wamekuwa na mapungufu mengi.

Kocha huyo ameisifia Ligi ya Tanzania akiamini kuwa ni bora zaidi lakini akitupa lawama zake kwa baadhi ya waamuzi wanaoifanya ipoteze mvuto.

Hajasita kuwashauri viongozi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) kujaribu kufuatilia mchezo wao wa jana walicheza na Stand ili kubaini madhaifu ya waliochezesha mechi hiyo.

Katika mechi ya jana ilikubali kupoteza mchezo wake wa kwanza kwenye msimu huu na kuwa sawa na Simba na Azam ambazo kila moja imepoteza mchezo mmoja.

9 COMMENTS:

  1. Ameanza kulaumu waamuzi .Hii ni trela.TFF hawataki kupanga mechi na Azam lakini mwisho itafikia tu.

    ReplyDelete
  2. Waamuzi ambao huchezesha mechi ambazo huwa unashinda huwa wanatoka ligi ya nchi gani? Au waamuzi wamekuwa sio bora kwa vile jana umefungwa?! Acha kupenda ambo mazuri yatokee kwako tu, hata hizo timu zingine pia zinapenda mambo mazuri ikiwamo kushinda. Kama ingekuwa imepangiwa Yanga peke yake kushinda, kungekuwa na maana gani ya ligi kushirikisha timu zingine 19? Si TFF wangekuwa wanawaita tu "Yanga njooni mchukue kombe", wewe unadhani timu zinapoteza gharama bure za maandalizi na usafiri!!!. Hujaumbwa kushinda tu bhana, kocha bora huwa anakubali matokeo.

    ReplyDelete
  3. Nyie mashabiki wa mbumbumbu mna midomo sana

    ReplyDelete
  4. Mwanaume kamili anakufa Vitani lakini teja anakufa Stendi. Tafakari.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani jana mlikuwa mnapambana au mlikuwa mnapigwa za uso tu? Hamkuwa mnapambana kwa sababu kama mngekuwa mapambanon mngeshinda atleaat 5/2, Lakini 5/0? Ni afadhali anayefia stend aisee

      Delete
    2. Sasa vile ni kufa vitani au mwanaume wa vita alikufuata chumbani ulikojificha na mkeo pamoja na watoto akakuchapa na kukudhalilisha mbele ya mkeo na watoto?.....ninaposema kudhalilishwa mbele ya mkeo nadhani nimeeleweka.

      Delete
  5. uwanaume gani wa kufa KHAMSA mmetutia aibu kufungwa ma VITA goli 5 - 0 mechi ya stand iangalie tena utaona offside za upendeleo na penalt alizonyimwa Yanga

    ReplyDelete
  6. Timu ipo ya 16 kwenye ligi unataka mbebwe. Bikira ndio imetoka hivyo.Hakuna penalti mliyonyimwa. Mlizoea kuwatisha marefa. Jana mngemsogelea refa mweledi Warioba kutoka Mwanza. Hamna upendeleo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic