January 24, 2019


Baada ya kufanikisha kuwatwanga Gor Mahia FC ya Kenya katika mashindano ya SportPesa Super CUP jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Naibu Meya wa jiji la Mwanza, Biko Kotecha, ametuma salaam za pongezi kwa Mbao FC.

Kotecha amesema salaam hizo ni watu wote wa Mwanza kwani walichokifanya Mbao kimeitangaza vema Tanzania na jiji la Mwanza kwa ujumla.

Ameeleza ushindi huo ni chachu ya kukuza mafanikio kisoka katika jiji la Mwanza na akiamini uwezekano wa kuwa na timu zingine kama Mbao utakuwepo.

Katika mechi hiyo, Mbao alifanikiwa kuibuka na ushindi wa matuta 4-3 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 1-1.

Mbao sasa imungana na Simba kuelekea nusu fainali ambapo timu hizo mbili zitakutana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic