January 9, 2019


Straika wa timu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta atatua katika Klabu ya Mid­dlesbrough ya England endapo klabu hiyo ikitoa kiasi cha Euro milioni 6.5 (bilioni 17) ambayo ndiyo thamani ya mchezaji huyo.

Samatta anayeongoza chati ya wafun­gaji katika Ligi Kuu ya Ubelgiji akiwa na mabao 15, anawindwa kwa ukaribu na baadhi ya timu za Eng­land sam­bamba na Fenerbahce ya Uturuki.

Kwa mujibu wa takwimu za Mtandao wa viwango wa Transfermarket, unaonyesha kwamba tha­mani ya nahodha huyo wa Taifa Stars imepanda maradufu kutoka ile aliyokuwa nayo Septemba, mwaka jana.

Kwa sasa Samatta anayeshika nafasi ya tano kwa ubora ndani ya kikosi cha Genk, amepanda thamani kutoka Euro milioni nne (sawa na bilioni 10), mwaka jana hadi bilioni 17 kwa mwezi huu.

Timu ambazo zinamtaka mshambuliaji huyo anayekama­ta nafasi ya 183 duniani kwa wachezaji wanaocheza nafasi ya mshambuliaji wa kati, zitalazimika kuilipa KRC Genk dau hilo la bilioni 17, kwa ajili ya kuipata huduma yake.

Wakati Samatta ambaye ndani ya Ligi kuu ya Ubelgiji akikamata nafasi ya 14 kwa ub­ora wa viwango vya wachezaji thamani yake ikipanda, swahiba wake Thomas Ul­imwengu aliyejiun­ga na JS Saoura ya Algeria, mam­bo hay­aendi sawa baada ya thamani yake kushuka kutoka dola 150,000 hadi dola 100,000

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic