Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha, hatimaye leo amezindua rasmi kampeni zake za kuwania nafasi ya mwenyekiti katika klabu hiyo.
Katika uzinduzi huo uliyofanyikia makao makuu ya klabu hiyo amewatambulisha baadhi ya wajumbe wanane atakaoambatana nao, ambao ni Ally Msigwa, Christopher Kashililika, Dominic Francis na Salim Rupia.
Wengine ni Arfat Hadji, Said Barala na Peter Simon ambao wote ni wagombea katika nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo.
Tiboroha ameanika vipaumbele vyake kuwa akipewa ridhaa ataanza na kujenga na kuimarisha taasisi hiyo, pili atafanya juhudi za haraka kuirudisha klabu kwa wanachama na mashabiki wake.
Pia amesema atafanya kazi ya kuimarisha matawi, atajenga mara moja misingi ya uwekezaji na biashara, kuimarisha na kujenga mifumo ya klabu na kushirikisha wadau wote.
Huyu hawezi kuiongoza Yanga alikuwa mpigaji kipindi kile!
ReplyDeleteAlipiga nini
DeleteDuh hili movie la kihindi ngoja tusubiri mwisho wake.
ReplyDeletealishindwa kuiongoza Stand united badala yake akazusha mgogoro hadi wadhamini wakajitoa
ReplyDeleteUongozi huu utaivusha Yanga
ReplyDeleteMwenyekiti: Dr. Mbaraka Igangula
M/Mwenyekiti: Yono Kevela
Wajumbe
Sylvester Haule
Athanas Kazighe
Salum Rupia
××××× ××××
Mfumo wa Kampuni kuanzishwa
CEO as Young Africans Sports Club Limited
Dr. Jonas Tiboroha
Bodi ya Wakurugenzi- Tarimba Abbas
Francis Kifukwe
Hamad Islam
Binklebu
Ramesh Patwa
Seif Magari
Mwekezaji
IPP au Rostam Aziz
ila nadhani Dr. Tiboroha ni mtu sahihi....kwa muda wa mwaka mmoja na nusu....
ReplyDelete