January 11, 2019


Mwekezaji mkuu wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji 'Mo' amewaomba amshabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba itashuka kesho Jumamosi kucheza na JS Saoura ya Algeria ukiwa ni mchezo wa hatua ya kwanza kwenye makundi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mo ameandika kuwataka wanasimba wote waende wakaupendezeshe Uwanja ili kuhakikisha timu inashinda.

Tayari kile kikosi cha kwanza kimesharejea Dar es Salaam kutokea Mapinduzi CUP Zanzibar ambako kilienda kusherehesha mashindano hayo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic