January 24, 2019




Mabingwa wa soka Tanzania, Simba wameshusha kifaa kingine, safarii ni mchezaji raia wa Namibia.

Imeelezwa ni mshambuliaji na jina lake halisi ni Sadney Urikhob na amewahi kucheza soka kwao Namibia na Afrika Kusini.

Pamoja na Afrika, Urikhob amekipiga barani Asia katika nchi za Indonesia, Malaysia na Vietnam.

Tayari yuko jijini Dar es Salaam na ameishaonana na kocha Patrick Aussems.

Simba inaonekana inataka kuimarisha safu yake ya ushambulizi kwa sababu ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Tayari wachezaji wawili kutoka Ghana na Togo wako Dar es Salaam na jana wameichezea Simba dhidi ya AFC Leopards katika michuano ya SportPesa Super Cup.


TAARIFA ZINAELEZA GAZETI LA SPOTI EXTRA LILILO MTAANI LEO ALHAMISI LIMENASA KILA KITU KUHUSIANA NA UJIO WAKE NA TIMU ALIZOKUWA AKIZICHEZEA.

5 COMMENTS:

  1. Wewe timu yako sio simba!Acha unafiki!
    AlJanuary 22, 2019 at 7:55 PM
    Kocha wa Yanga hana mbinu anaongea sana na vyombo vya habari badala ya kujikita kukisuka kimbinu timu yake.....watu wanaaminishwa ubora wa timu lakini kiuhalisia beki mbovu sana hata golikipa hawana formation ya kucheza kwa mbinu....Kocha msanii sanii tu Kombe hili anachukua Simba au Gor Mahia. Yanga wasipofanya mageuzi katika beki na viungo vyao jinsi wanavyocheza na kukaba pindi wanapoteza mpira wataendelea watapoteza mechi nyingi....KAMA NI MDAU WA YANGA UNASOMA UJUMBE HUU FIKISHA KWA HARAKA SANA UJUMBE KWA

    ReplyDelete
  2. Bado mimi nalia na mchezaji anae weka kukata umeme pale katikakti akisaidaina na Kotei na Mkude...... tukipata huyo mtu tumemalza..

    ReplyDelete
  3. Huyu Mnamibia ni bonge la straika kama atakuwa yupo fiti yaani hana injury au matatizo menginebya kiafya nashngaa Simba wanajichelewesha kumfanyia majaribio yanini mtu Sydney? Wanatakiwa kumfanyia John Boko majaribio kwanza sio kwa mchezaji kama Sydney ni mchezaji wa kulazimisha haraka haraka kabla haijatokea klabu nyengine ikamnyakua.

    ReplyDelete
  4. Wacha kumsifia huyo Sadney.Aonyeshe uwezo uwanjani .Aliumia goti kuna uhakika amepona kabisa?
    Hajachezea timu ya Taifa ya Namibia kwa muda sasa.
    Simba kuweni makini msifanye usajili wa pupa .

    ReplyDelete
  5. Simba mjithatiti xan nausajili wenu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic