January 9, 2019


Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, amempiga dongo Msemaji wa Yanga, Dismas Ten kuhusiana na matumizi ya Kompyuta Mpakato 'Laptop'.

Manara amesema hayo wakati wa kikao na waandishi wa habari jana kunako makao makuu ya Simba kuelekea mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura ya Algeria.

Katika kikao hicho Manara alieleza kuwa atahakikisha anakaa jukwaa la mashabiki siku ya mchezo na kuachana na VIP ili kuongeza hamasa kwa mashabiki hao.

Dongo kwa Ten lilikuja baada ya kusema yeye si Ofisa Habari anayekaa na Laptop muda wote bali yupo kwa ajili ya kuweka hamasa kwa mashabiki ili wajitokeze kwa wingi Uwanjani.

Kauli ya Laptop imekuja kutokana na Ten ambaye pia amekuwa akimkejeli Manara kuwa hana uzoefu wa kutumia Laptop hivyo naye akaona ampe kijembe jana mbele ya wanahabari.

6 COMMENTS:

  1. wewe kama msemaji(mwanahabari)wa timu kuwa na vitendea kazi kama laptop ni kitu cha kawaida,labda ungekuwa wazi kuwa hujui kuitumia ndo mana huonekani nayo hiyo ingeleta maana.Kwa tafsiri yako ni kwamba kuwa msemaji/mwanahabari wa simba ni kwenda kukaa jukwaa la mashabiki na kushangilia nao......your wrong brother.Hicho unachokifanya wewe siku zote si u-wanahabari....,ukiniambia au wakiniambia kuwa wewe ni muhamasishaji wa klabu ntakuunga mkono kwa asilimia mia moja kwakuwa kazi hiyo unai-fit vizuri.Hivyo itakuwa ni jambo jema kama simba watatafuta mtu mwingine wa habari atakaekuwa na weledi wa habari kama akina D10 ili wewe uendelee na fani yak0 ya uan-hanabri.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ni hoja zako ambazo kwa wengine hazina mashiko.Dismas anapaswa kuamka naye ili ainue brandy ya Yanga badala ya kututangazia mwezi huu tumeingiza laki tisa baada ya kutembeza mabakuli hadi imefikia kocha anatoa pesa yake mfukoni.Is shame!!!

      Delete
  2. Zahera anahamasisha zaidi ya mwenye kazi hiyo pale yanga.

    ReplyDelete
  3. Manara ni mkuu wa kitengo cha habari. Akitembea ba laptop wasaidizi wake wafanye nini?
    Manara anafanya kazi nzuri sana ya kukuza brand ya Simba.
    Ndio maana unaona Zahera ametake over kazi za Dismas.Hawezi hata kuongea sijui jukumu ni kubwa sana kwake au ushamba.
    Mimi ni Yanga lakini natamani tuwe na msemaji kama Manara.

    ReplyDelete
    Replies
    1. zibitsha uyanga wako achana na kauli za mi yanga

      Delete
  4. Namba yangu ya uanachama ni 2146.
    Bado unabisha ????

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic