January 9, 2019


Kuelekea uchaguzi wa kujaza nafasi katika klabu ya Yanga ambao unatarajia kufanyika Januari 13 2018, Mgombe nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Magege Chota, ameahidi kulipa fedha zote za mishahara endapo atachaguliwa.

Chota ameeleza kuwa Yanga hivi sasa inapitia wakati mgumu kiasi cha kwamba wachezaji wamekuwa wakicheza bila kutimiziwa stahiki zao.

Ameeleza suala hilo litakuwa ni la kwanza kuanza kulitekeleza ili kuondoa mkanganyiko uliopo hivi sasa ndani ya kikosi ambapo kuna baadhi ya wachezaji wamekuwa wakigoma.

Mwanachama huyo ameanza kampeni zake rasmi baada ya hapo jana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuthibitisha kuwa muda wa kampeni umeshaanza na utachukua siku tano.

"Unaua wachezaji wa Yanga wengi hawajalipwa fedha za mishahara yao, nawaahidi wanachama wa Yanga kuwa nitafanya zoezi la kuwalipa wachezaji ili vita ya mapambano ishike kasi endapo wakinipa kura" alisema.

2 COMMENTS:

  1. Angetuambia kwanza hizo pesa za kuwalipa atazitoa wapi

    ReplyDelete
  2. Hao ni Aina ya Viongozi tusiowataka Yanga na kamati ya Uchaguzi hiangalie kampeni hii, Huo ni ushawishi was kutumia hela kupata mafadaraka nawala Asemi atatumia siku ngapi kulipa,isije akalipa kupitia viingilio vya mechi, yy aseme akipata Uongozi atatumia siku ngapi kulipa malimbikizo ya madai ya Wachezaji na benchi la ufundi.?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic