BAADA ya Yanga kupoteza mchezo wao wa leo kwenye kombe la Mapinduzi kwa kufungwa mabao 3-0 uliochezwa Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar, nahodha wa mchezo wa leo Deus Kaseke amesema kilichowaponza kufungwa ni kukosa umakini.
Kaseke amesema kuwa ushindani ni mkubwa na kila timu inatafuta matokeo hivyo kushindwa kwao kupata matokeo ni sehemu ya matokeo na wanajipanga kwa ajili ya mchezo ujao.
"Tumetengeneza nafasi nyingi hatujazitumia tofauti na wenzetu ambao wametengeneza nafasi na wakatumia, kwenye mpira inatokea, hivyo mwalimu ameona mapungufu yetu na tutafanyia kazi," alisema Kaseke.
Agrey Moris nahodha wa Azam FC amesema kuwa upinzani ulikuwa mkubwa kutokana na timu zote kutoka bara, hivyo ni mwanzo mzuri.
" Kikubwa ambacho sisi kwetu tunaangalia ni kupata pointi tatu bila kuangalia idadi ya mabao tutakayofunga, tunashukuru tumepata matokeo tutaendelea kupambana," alisema.
Azam anaongoza kundi B akifuatiwa na Malindi wote wakiwa na Pointi nne, Yanga anashika nafasi ya tatu akiwa na pointi tatu, KVZ nafasi ya nne akiwa na pointi nne na nafasi ya tano inashikwa na Malindi ikiwa na pointi moja.
Mkiambiwa makanjanja mnafuta comments za watu.Someni tena hiyo aya ya mwisho .Inaeleweka?Hamfanyi editing?
ReplyDeleteha saleh Jembe.AIBU! akicheza Yanga mnafuatilia hadi SAA nne mnatoa kilichoendelea. Simba ikicheza inafika hadI SAA tano asubuhi siku inayofuatia hamjatoa matokeo ya mchezo...Haya kikosi chenu mlichokiita cha wanaume Leo hoi..
ReplyDeleteEti hawataki poteza nguvu kwenye mashindano ya mil 15..December kopo LA omba omba liliingiza mil 3..sasa si hela hiyo ya miezi tano ya omba omba.Itakuwa kama kujitoa sportpesa ili kujiandaa shilikisho na huko wakafungwa na timu zote walizokutana nazo
ReplyDeleteKiuhalisia kupeleka kikosi cha vijaba ni waliikwepa tu Simba!
ReplyDeleteHawa jamaa mi nawaitaga WANARIADHA.Kila siku wanawaza kumkimbia Simba
ReplyDeleteUmeandika "...Azam anaongoza kundi B akifuatiwa na Malindi wote wakiwa na Pointi nne, Yanga anashika nafasi ya tatu akiwa na pointi tatu, KVZ nafasi ya nne akiwa na pointi nne na nafasi ya tano inashikwa na Malindi ikiwa na pointi moja." UMECHEMSHA.
ReplyDeleteUmeandika na kutuaminisha kuwa KVZ nafasi ya 4 points 4, Yanga nafasi ya 3 points 3, Malindi nafasi ya 2 pointi 4 , Malindi tena nafasi ya 5 pointi 1. Fanya tathmini na urekebishe habari yako.
Delete