January 8, 2019


USHINDI wa mabao 2-1 dhidi ya KVS walioupata Azam FC katika Uwanja wa Amaan, umemuibua Kocha Msaidizi wa  wa Azam FC, Juma Mwambusi na kusema kuwa aliwaambia wachezaji wake wacheze mpira na kutafuta ushindi waachane na mwamuzi.

Mwambusi  amesema kikosi cha KVS kina wachezaji wenye uzoefu na wenye juhudi za kutafuta matokeo Uwanjani hali iliyowafanya wawe na subira kupata matokeo katika mchezo huo wa Kombe la Mapinduzi mpaka kipindi cha pili.

Mwambusi amesema mbinu kubwa aliyoitumia ni ya kiufundi hasa kwa kufanikiwa kufanya mabadiliko ya mchezaji wake Donald Ngoma ambaye aliingia na kubadilisha matokeo.

"Mbinu kubwa ya kiufundi imetumika, niliwaambia wachezaji wanapaswa watafute matokeo bila kujali kwamba tupo nyuma bado tuna nafasi ya kupata matokeo.

"Hali ya joto ilikuwa inawasumbua wachezaji pia walikuwa wanataka kucheza na mwamuzi ndio maana kulikuwa na ugumu wa kupata matokeo ila kitu kizuri walifanikiwa kufuata maelekzo na kubadili upepo wa mchezo," alisema Mwambusi.

KVS waliandika bao la kwanza dakika ya 16 kupitia kwa Amour Bakari Ali huku Azam FC wakiandika mabao kupitia kwa Donald Ngoma dakika ya 75 na Obrey Chirwa dakika ya 90.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic