KIKOSI cha Yanga kimeonyesha ubora wake ndani ya Bongo baada ya kufanikiwa kutwaa tuzo tano msimu huu zinazoandaliwa na Kamati ya Tuzo iliyo chini ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Tuzo hizo ambazo lengo lake kubwa ni kuendeleza ushindani ndani ya ligi, kwa msimu huu wa 2018/19 Yanga wamefanikiwa kufanya vizuri kutokana na watu wao wawili kuzibeba tuzo tano.
Tuzo ya kwanza aliichukua kocha mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera baada ya kuchaguliwa kuwa kocha bora mwezi Septemba, kocha huyo akachukua tuzo hiyo tena mwezi Novemba na Desemba.
Wakati Zahera akibeba tuzo hizo tatu, mshambuliaji wa timu hiyo, Heritier Makambo naye amefanikiwa kubeba tuzo mbili za mchezaji bora katika ligi hiyo.
Alianza kubeba tuzo ya mwezi Novemba, kisha Desemba akachukua tena.
Mpaka sasa zikiwa zimetolewa tuzo za mwezi Agosti, Septemba, Oktoba, Novemba na Desemba, Yanga ndiyo imeonekana kuwa kinara wa kuzibeba tuzo hizo.
Kutoka Championi
0 COMMENTS:
Post a Comment