January 7, 2019


Imeelezwa kuwa sakata la Kipa wa Yanga, Beno Kakolanya limefika kwa Mwanasheria ili kujua kama kutakuwa na uwezekano wa kuvunja mkataba.

Taarifa imeeleza kuwa kwa Mujibu wa Meneja wa Kakolanya, Haroub Seleman, amefunguka kuwa suala hilo limefika huko na linafanyiwa kazi.

Seleman amefunguka wanachoangalia hivi sasa ni kujua namna wanaweza kuvunja mkataba dhidi ya Mwajiri wake ambaye ni Yanga kutokana na kukosa maelewano mazuri.

Meneja Seleman amesema kilichoepelekea maamuzi hayo kufanyika ni kukosekana kwa maelewano dhidi ya Kakolanya na Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera hivyo hawanoni haja ya kuendelea kuichezea Yanga.

Taarifa zinasema kuwa mpango uliopo hivi sasa ni kuvunja mkataba kisha kumtafutia mchezaji huyo timu nyingine ambayo si ya hapa Tanzania bali ni nje ya nchi.

4 COMMENTS:

  1. Huyu kakolanya jinga sana. Huuwezi kuwa kwenye kundi la watu 10 wanaodai hela halafu wewe ugome wakati wenzio hawajagoma huko ni kujitoa sadaka. Ona sasa anataabika kucheza huchezi mkataba unamfunga na hela hujapewa. Sasa kapata nini? Kapata kapoteza.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sio mjinga..ila hao wasioomba haki ndio wajinga

      Delete
  2. Makipa wa BONGO hawanaga soko nje, msijidanganye.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic