January 10, 2019





Msafara wa kikosi cha JS Saoura cha Algeria umetua usiku huu jijini Dar es Salaam ikiwa ni maalum kwa ajili ya kupambana na wapinzani wao Simba.

Msafara huo wa zaidi ya watu 30 ukiwajumuisha wachezaji, makocha, waandishi wa habari na viongozi wa timu hiyo umetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ukitokea kwao Algeria.

Katika msafara huo yupo staa Mtanzania, Thomas Ulimwengu ambaye aliwaongoza wachezaji wa kikosi hicho baadhi ya mambo.

Akizungumza mara baada ya kutua uwanjani hapo Ulimwengu alisema: "Nina furaha kurudi kucheza tena nyumbani, Simba ni timu nzuri lakini sisi tumejiandaa kwa ajili ya kupambana nao."

JS Saoura watacheza na Simba katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi hii katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic