January 10, 2019


Baada ya msafara wa kikosi cha JS Saoura cha Algeria kutua usiku huu jijini Dar es Salaam, baadhi ya viongozi wameonyesha kujiamini.
Baadhi ya maofisa wa Saoura walionyesha kujiamini na kunyoosha vidole, wakimaanisha watashinda kwa mabao mawili.

Mbwembwe hizo ziliendelea wakati wakipakia maji na baadhi ya vyakula walivyokuja navyo.

Saoura na Simba watakipiga keshokutwa Jumamosi kwenye dimba la Uwanja wa Taifa ikiwa ni mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya makundi.






1 COMMENTS:

  1. Kwanza Ahsante sana Simba kwa kutufikisha hapa tulipo ni vigumu kukubali lakini Simba wanaitangaza nchi kwa namna moja au nyengine kwa hivyo ni vyema wakapewa sapoti ili waendelee kufanya hivyo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic