KOCHA wa timu ya Lipuli, Seleman Matola amesema kuwa mwenendo wa mzunguko wa pili kwa timu nyingi zinazoshiriki Ligi Kuu ni mbaya kutokana na ugumu wa uendeshaji wa timu.
Matola amesema kwamba kutokana na kukosekana mdhamini mkuu kwenye Ligi, timu nyingi zinashindwa kujiendesha hali ambayo imefanya mtindo wa bakuli kupata umaarufu msimu huu.
"Wadau wengi kwa sasa wanashindwa kutoa sapoti kwa timu zao haina maana kwamba hawapendi hapana ila ni ugumu wa uchumi ulivyo na mambo kuwa mengi ndo maana unaona timu nyingi zinaombaomba.
"Kuna umuhimu wa kuwa na mbinu mbadala kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na wadau kutoa sapoti kubwa ili kuweza kuziendesha klabu kwani kwa sasa hali sio shwari hasa kwa baadhi ya timu ambazo hazina hata mdhamini," alisema Matola.
Ligi Kuu Bara msimu huu inaendeshwa bila mdhamini mkuu kutokana na yule aliyekuwa akidhamini mwanzo kushindwa kuendelea kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi na TFF.
0 COMMENTS:
Post a Comment