January 24, 2019



Baada ya jana kufanikiwa kuwang'oa mabingwa watetezi wa SportPesa Cup Gor Mahia, uongozi wa Mbao FC umesema nguvu zao kwa sasa ni kwenye hatua ya nusu fainali itakayochezwa kesho Uwanja wa Taifa.


Hii ni mara ya kwanza kwa Mbao kushiriki michuano ya SportPesa Cup na wameleta ushindani kwa kufika nusu fainali na kesho watacheza na KK Sharks.


Katibu mkuu wa Mbao, Daniel Naila amesema wana furaha kufika hatua ya nusu fainali hesabu zao ni kuona wanapata matokeo chanya na kufika hatua ya fainali.


"Ni jambo la kheri kwetu maana tuliahidi tangu awali kuleta ushindani na tumefanikiwa, kwa sasa hesabu zetu ni nusu fainali.

"Tunatambua KK Sharks ni timu nzuri tumejipanga, tunaamini tukivuka hatua ya nusu fainali tunatinga fainali lengo ni kuona tunabaki na kombe nyumbani msimu huu," alisema Naila.

1 COMMENTS:

  1. Mjadala mkubwa unatakiwa kulinusuru Soka la Tanzania....kuanzia TFF Bodi ya Ligi kuna yafuatayo ambayo yanaua soka
    1. Ubadhirifu wa Pesa,Wizi, madeal ya wajanja wajanja katika kuuza na kuingia mikataba ya jezi na Matumizi mabovu ya pesa (Vyama vya Soka mpaka Klabu)
    2. Rushwa katika Waaamuzi wa Soka ngazi zote
    3. Upangaji mbovu wa Ratiba za Michezo ya Ligi huku baadhi ya timu zikipewa upendeleo maalumu kwa sababu ya upenzi wa Baadhi ya Viongozi wa Soka
    4. Kutokuwa udhamini wa mashindano, hakuna sera na viongozi wenye weledi na wanaojua kutafuta vyanzo vya mapato na masoko kwaajili kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa timu za mpira wa miguu
    5. Hakuna ushirikiano wenye tija kati ya TFF na vilabu vyote....baadhi ya vilabu hasa vya Dar Es Salaam kupata "preferential treatment" over others....

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic