January 31, 2019


BIASHARA United ya Mara leo watakuwa wageni mbele ya Yanga uwanja wa Taifa wakicheza mchezo wa shirikisho ikiwa ni hatua ya nne kwa mujibu wa Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema wachezaji wote wana morali na wapo sawa.

Mchezo wa leo Biashara United kwa mara ya kwanza tangu wapande Ligi Kuu Bara watakuna na mtambo wa kutengeneza mabao Yanga, Ibrahim Ajibu mwenye mabao 6 na pasi za mabao 14 kwenye Ligi Kuu Bara.

Kwenye mchezo wao wa kwanza waliokutana nao ambao ulikuwa ni wa Ligi Kuu Bara Uwanja wa Taifa, Ajibu aliwakosa Biashara kutokana na matatizo ya kifamilia licha ya kutokuwepo walishinda mabao 2-1.

Pia kiungo mwenye uzoefu na Ligi kuu pamoja na michuano ya kimataifa, Mrisho Ngasa naye pia leo atakutana na Biashara kwa mara ya kwanza kwani walipokutana kwenye Ligi Kuu alikuwa anatumikia kadi nyekundu aliwakosa Biashara United.

Biashara United wao wana kocha mzoefu Amri Said ambaye alikuwa wa kwanza kuitungua Simba alipokuwa Mbao na sasa yupo na kikosi cha Biashara hivyo anakuwa ni mpya kwa kikosi cha Yanga kwani wakati Biashara inafungwa ilikuwa chini ya kocha Hitima Thiery.

Ajibu ataingoza Yanga leo akiwa ni nahodha mkuu kwa mara ya kwanza kwenye kombe la FA, huku ile ya Ligi akiwa amefanya hivyo mara mbili akipoteza mmoja na kushinda mmoja.

Pia mtambo wa mabao wa Yanga FA, Amiss Tambwe yupo fiti pia kuanza leo kuendeleza ubabe wake ndani ya Uwanja wa Taifa ambao rekodi nao.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic