January 8, 2019


Acha kabisa!! Imeelezwa Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amekunwa kinoma na kiwango cha Mshambuliaji wa Simba, Mghana, Nicholas Gyan.

Aussems ameonekana kufurahishwa na kiwango cha mchezaji huyo huku akimwelezea kuwa amezidi kuimarika kadri siku zinavyoenda.

Gyan ambaye wakati wa Joseph Omog hakuwa anapata nafasi, mpaka sasa amekuwa na fomu nzuri kwenye mashindano hayo yanayoshika kasi visiwani Zanzibar.

Kukua kwa kiwango cha Gyan kumemfanya Aussems amsifie na kuamini akiendelea kupambana atakuwa vizuri zaidi.

Katika mchezo wa mwisho wa Mapinduzi ambao Simba walicheza dhidi ya KMKM, walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 likifungwa na Rashidi Juma.

2 COMMENTS:

  1. Tuwache utani Gayani ni moja ya vipaji halisi kati ya vingi vilivyojazana ndani ya Simba. Kama alivyosema kocha yakwamba kama Gayani ataendelea na hali ya kujiamini aliyonayo hivi sasa basi kwa wenzetu hawa watu wa magharibi mwa Africa tutarajie kumuona mbali zaidi. Nadhani viongozi na hasa mashabiki wa mpira Tanzania tujifunze na baadhi ya matukio kama ya Chirwa na sasa Nicholasi Gayani yakwamba wakati mwengine watu wanatakiwa kuwa na subira kuliko kukimbilia kukihukumu kiwango cha mchezaji. Papara kama hizo ndizo zilizowafanya Chelsea kwaachia Mohamedi Salah na Lukaku na wengine wengi. Na hata Manchester United iliwalazimu kukunjua mkwanja mrefu kuyarejesha matapishi yao ya Pogba. Kwa maoni yangu naona hata akina kaheza kulikuwa hakuna haja ya kuwatoa kwa mkopo sema kocha ndio kaamua. Simba ya sasa ni mahala sahihi kwa makuzi ya wachezaji wenye vipaji kuliko timu nyingi katika ukanda wetu huu na ni vizuri vujana waliopo ndani ya kukomaa kweli kweli kuhakikisha kama kuondoka kwao Simba basi iwe kukubwa zaidi sio mkopo au kufeli.

    ReplyDelete
  2. Anafaa kucheza nafasi za forward na hasa nyuma ya center foward ama sambamba na forward. ppia jamaa alinesha interest ya kuchezea national team, hata kw a kubadili uraia wa nchi nyingine. sasa nadhani ni fursa kwa sisi watanzania kuwachukua watu w namna wenye vipaji, nia na shauku km hii. kwa Timu yao ya taifa pale Ghana hawezi kupata nafasi kwa ss labda baadae sana, ila hapa bongo nafasi anayo. Tena hawa jamaa wanajituma sana anaweza kwani anaweza kupata klabu nje na kutoka hata nje ya nchi kucheza soka ktk vilabu vya nchi zilizopiga hatua huku ni raia wa Tanzania mwenye nafasi ya kuchezea timu ya Taifa. Tuwape tu nafasi ya uraia watu kama hawa. Hii huenda ikasaidia kuvuta vipaji vingne nje ya nchi ambao hawana nafasi ktk national team na kuchukua uraia ili waongeze nguvu nations team. njia hii huenda ikatuondoa hapa tulipo na kutusogeza kupiga hatua (mfano nchi ya Ufaransa). Jambo hili yawezekana wenzetu majirani wakatucheki ila mbeleni wakaja kutuheshimu baada ya mafanikio ya timu ya Taifa kupatikana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic