YANGA WATAKA MCHEZAJI AFUTWE KAZI MARA MOJA
Baada ya kupoteza kwa mabao mawili kwa moja na kuondolewa kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi huko Zanzibar, baadhi ya mashabiki wa timu hiyo wameijia juu ya Kamati ya Usajili Yanga.
Mashabiki hao baadhi ambao hawakutaka majina yao yatajwe, wameitaka Kamati hiyo kukaa chini na kutakafakari mara moja kwanini walimsajili kipa Ibrahim Himid wakati haendani na hadhi ya klabu.
Wameeleza kuwa kwa namna kiwango chake kilivyokuwa kimesababisha Yanga kutolewa mapema jambo ambalo wengi hawajalifurahia.
Katika mabao mawili aliyofungwa yameonekana kuwa ya aina moja jambo ambalo mashabiki hao wamekerekwa haswa na uwezo wa Hamid.
Aidha wameenda mbali zaidi wakiomba ni vema kama ikiwezekana kipa huyo avunjiwe mkataba wakiamini anaweza akailetea aibu Yanga huko mbele ya safari.
EtiCannavaro timu yenyewe imebaki Dar?
ReplyDeleteHivyo ni visingizio tu! Kila timu hutoa vyake ikifungwa..Simba walipoondolewa na Mashujaa walidai eti sio kikosi cha kwanza kilicheza..Jana Liverpool imepigwa na wolves wanadai walichezesha watatu ambao ni under 18.Hakuna timu ambayo wanahitaji Mil 15 kuzidi Yanga.Wangepeleka kikoosi cha kwanza wangeweza kuzipata kuliko kutembeza kopo unaishia laki 9 katika mwezi mmoja
..������������ na badooo
ReplyDeleteWamwache hukohuko Zanzibar si keshafika kwao? Hana kiwango cha kudaka sio Yanga tu hata timu yoyote inayocheza premier
ReplyDeleteSajili za bongo zinafanywa kwa mkumbo,mayowe na makelele ya mashabiki majukwaani. Ukibahatisha kupangua shut kali watu wakashangilia unasajiliwa.
ReplyDeleteUkiwauliza waliompendekeza asajiliwe walimfuatilia Michezo mingapi utakuta hata hawamfahamu nao wametajiwa au ndio walimuona siku hiyo wakavutiwa nae
ReplyDeletePamoja na hayo huwezi kusajili kizuri wakati huna pesa ndiyo maana tunaokotaokota tu.
ReplyDelete