KIKOSI cha Mbao, kilicho chini ya Kocha Msaidizi Ally Bushiri kitakuwa kwenye kibarua kizito kupambana na Alliance FC ambayo kwa sasa imeanza kushika kasi katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa leo Uwanja wa Nyamagana.
Mbao itacheza na Alliance ikiwa na kumbukumbu katika mchezo wao wa kwanza kushinda kwa bao 1-0 lilifungwa na Evargritius Mujahukwi ambaye aliingia Uwanjani akitokea benchi.
Ofisa Habari wa Alliance, John Mwafulango amesema kikosi chake ni imara kutokana na kucheza soka la kwenye kitabu hawana hofu na wapinzani wao watasambaza upendo wa misumari ya mabao.
Mwenyekiti wa Mbao, Solly Njash amesema upinzani uliopo hauwapi hofu kwani wana kikosi imara ambacho kinatafuta matokeo chanya Uwanjani.
0 COMMENTS:
Post a Comment