MCHEZAJI YANGA AUNGANA NA ZAHERA KUMPIGA CHINI UNAHODHA YONDANI
Aliyewahi kuwa mchezaji wa Yanga hapo zamani na sasa Mchambuzi wa masuala ya soka, Ally Mayay, ameungana na maamuzi ya Kocha Mwinyi Zahera kumvua Kelvin Yondani unahodha.
Zahera alimvua Yondani kitambaa cha unahodha baada ya kusema kuwa mchezaji huyo amekuwa hana mwenendo mzuri wa nidhamu na kumkabidhi Ibrahim Ajibu.
Maamuzi hayo yamemuibua Mayay na kusema nidhamu ni suala la msingi kwa mchezaji hivyo pale inapotokea haitendewi haki ni vema hatua zikachukuliwa na Mwalimu kwenye kikosi.
Mayay amesema kuchukua kitambaa hicho kwa Ajibu kutaisaidia Yanga kutokana na mchezaji mwenyewe ana ushawishi mkubwa nje na ndani ya uwanja.
Mchambuzi huyo ameeleza Ajibu amekuwa na hamasa kubwa hivyo anaona ataweza kuwaongoza vizuri wenzake ndani ya Yanga ambayo ndiye inashika usukani wa ligi hivi sasa.
"Naimani Ajibu atakifanyia kazi vema kitambaa cha unahodha, maamuzi ya Zahera kumnyang'anya kitambaa Yondani yanategemeana na nidhamu ya mchezaji, kama alikosea basi Kocha yuko sahihi" alisema.
Kwani na huyo Ajibu si aliekuwa daima anagomea mazoiezi na pia kushiriki kucheza au ndio ksahau?
ReplyDeleteyeye ndo yuko na wachezaji siku zote,hivyo anaelewa yupi yuko vizuri kitabia kwa kipindi hiki na yupi hayuko vizuri......sio kama wewe unaemwangalia mchezaji kwa nje ambapo hujui kwa ukaribu maisha yake yapoje.........Na hata kama Utataka kulazimisha ajibu aendelee kuonekana mtovu wa nidhamu,bado kocha hajakosea,kwani kuna ule msemo usemao"MCHAWI MPE MWANAO AKULELEEE"
ReplyDelete