January 11, 2019



KIKOSI cha Yanga kimeendelea kufanya mazoezi ya kujiweka fiti katika Uwanja wa Polisi uliopo Kurasini kwa ajili ya mzunguko wa pili ambapo Jumanne watakuwa Uwanja wa Taifa dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga.

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema lengo lake kwa wachezaji ni kuona wanapata matokeo chanya kwenye michezo yote watakayoshuka Uwanjani ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.

"Wachezaji wanajua kwamba mashabiki wanaipenda timu yao na furaha yao imebebwa kwenye matokeo mazuri, hivyo hawana budi kucheza kwa umakini na kupata matokeo katika mechi ambazo tunacheza.

"Natambua ugumu wa kucheza na timu ambazo zina pointi chache ni ngumu sana kupata matokeo chanya endapo wachezaji hawataonyesha juhudi, nina imani tutapata matokeo," alisema.

Yanga wanaanza mzunguko wa pili wakiwa na kiporo cha mchezo mmoja mkononi dhidi ya Azam FC ambao wanashiriki kombe la Mapinduzi, Yanga wanaongoza Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 50.

2 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Kwahiyo baada ya hizo kesi za kuzuia uchaguzi kuchaguliwa, maana yake Manji anarudishwa....vyovyote vile itakavyokuwa Yanga inaonekana ni Imara....Manji anaendelea kusaidia Timu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic