January 11, 2019


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema anatambua ugumu wa mchezo wake wa kesho dhidi ya waarabu kutoka Algeria, JS Saoura ila ana imani na kikosi chake kitafanya vizuri kupata matokeo kwa kuwa anajua mbinu za wapinzani wake.

Kesho Simba watakuwa Uwanja wa Taifa kucheza mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa wakiwa kundi D ambalo lina timu kama Al Ahly ya Misri, AS Vita ya Congo na JS Saoura ya Algeria ambayo kesho itaanza kucheza Uwanja wa Taifa.

"Timu nyingi za kiarabu nazitambua hasa kutokana na uzoefu nilionao, nimefuatilia namna ambavyo wanafanya  na nimegundua kwamba wachezaji wao ni wajanja sana wanapiga sana kelele wakiwa uwanjani na wana mtindo wa kujiangushaangusha hilo lipo wazi nimeligundua na nimelifanyia kazi," alisema.

JS Saoura wametua jana Usiku wakiwa wameongozana na mtanzania Thomas Ulimwengu ambaye amesajiliwa msimu huu, huku wakiwa wamebeba maji yao pamoja na chakula chao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic