January 23, 2019


KOCHA wa timu ya Simba, Patrick Aussems amesema atatumia michuano ya SportPesa Cup kuwafanyia majaribio wachezaji wake wapya Moro Lamine raia wa Ghana na Hunlede Abel raia wa Togo ili aone uwezo wao kabla ya kusajiliwa.

Aussems amesema hana namna nyingine kwa sasa ili kukijenga kikosi chake kimataifa zaidi ya kufanya usajili makini ambao utaleta matokeo bora katika mechi za kimatifa kutokana na uhitaji uliopo ndani ya kikosi.

Aussems amesema kumpima mchezaji peke yake kwenye mazoezi haitoshi ni lazima pia awapime kwenye mechi na tayari ameomba nafasi tatu kwa uongozi kuweza kuwasajili ndani ya Simba.



"Kikosi changu kinahitaji marekebisho kwa kuboresha baadhi ya nafasi ikiwa ni pamoja na mshambuliaji mmoja na beki wa kati, lazima nifanye usajili wa wachezaji wenye uzoefu wa michuano ya kimataifa.

"Kabla ya kuwasajili wakiwa wanaendelea na mazoezi nimewapa nafasi ya kuwatumia katika michuano ya SportPesa Cup ambayo sisi tutaanza kucheza na AFC Leopards na tayari tumeomba ruhusa TFF na sheria zimeturuhusu, pia kuna mshambuliaji mwingine anatarajia kuja akitokea Benini," alisema.

Wachezaji ho leo watakuwa sehemu ya kikosi kitakachoanza kucheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya AFC Leopards ikiwa ni hatua ya robo fainali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic