January 18, 2019


Lile sakata la kipa wa Yanga aliyepigwa chini na Kocha Mwinyi Zahera limeibuka tena baada ya Mwanachama Mwandamizi, Edgar Chibula kuamua kuvunja ukimya.

Kwa mujibu wa Radio One, Chibula ameutaka uongozi wa Yanga kumfikiria Kakolanya kwakuwa bado ana mkataba na Yanga.

Mwanachama huyo ameeleza kuwa ni kweli Kakolanya alikosea lakini inabidi ifikie muda afikiriwe kama binadamu.

Ameongeza kuwa kipa huyo bado ana mkataba na Yanga na vilevile yupo katika kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars hivyo ni vema akafikiriwa upya.

"Ni kweli Zahera hana hamu ya kumsahe Kakolanya, lakini nauomba uongozi ujaribu kumfikiria mchezaji huyu kwa maana ana mkataba na vilevile anaichezea Taifa Stars" alisema.

5 COMMENTS:

  1. Edgar Chibula....!!!Kumbuka Beno Kakolanya hajafukuzwa ila alijiondoa yeye mwenyewe...sasa nini cha kufanya endapo yeye Beno ameogoma hata tu kutuomba radhi sisi washabiki, wanachama na hata wapenzi wa Yanga????
    Niliwahi kutoroka shule nikiwa kidato cha pili na kurudi nyumbani baada ya kuona shule hainiridhishi kielimu...kuanzia mwezi wa sita hadi wa kumi Baba yangu hakutaka hata kuniuliza tena kuhusu shule. Mimi mwenyewe ilipofika mwezi wa kumi nikaamua kubeba begi na kurudi shule..hakuna aliyenilazimisha. Sasa Beno anatakiwa yeye mwenyewe bila kupitia kwa wadau ajitokeze. Na mbaya zaidi alishaandika barua ya kuvunjiwa mkataba. Ni kikanuni barua ikikaa siku kumi na nne (14)..mkataba unakuwa umevunjika automatically. Beno keshavunja mkataba na Yanga kutokana na maongezi yake yeye mwenyewe Chibula

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umemaliza kila kitu sitii neno zaidi ya kuongeza maswali ya kufikirika.
      1. Je Beno alipoishitaki club TFF na TFF kutoa maamuzi yake ile kamati imefuta maamuzi?
      2. Beno aliandika barua ya kuvunja mkataba na Yanga je ameiondoa ile barua ?
      3. Beno alipopigiwa simu na kocha kitu gani kilimfanya asipokee akamueleza kocha kinachomsibu?
      4. Wale waliompatia Beno pesa kwenye chumba cc hatukijui hawafahamu ofisi za Yanga? je Hawafahamu kuwa wanaodai club ni wachezaji wote?

      Delete
    2. Eleweni kila mchezaji ana mkataba wake na klabu kwa maana haifanani.Mkataba wa Ngassa haufanani na wa Ajib, Yondani.Pengine kuna wachezaji wana mkataba wa kuchezea klabu kwa kulipwa posho tu.Eleweni mkataba kati ya muajiri na mwajiriwa ni siri.Usimlazimishe Punda kuvuka mto kwa kuwa simply unamtumia kwa manufaa yako.Wacha sheria ichukue mkondo wake!!

      Delete
    3. Ushamaliza kila kitu sina cha kuingeza zaidi ya kupiga tiki. Ila tatizo ni kwamba tunaangalia sana maslahi ya timu bila kumjali mwajiliwa mi naona beno yuko sahii

      Delete
  2. Endeleen kumpotosha, na ninyi mnaosema beno yupo sahihi ndiyo mliyomsabishia hayo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic