LICHA ya kupata ushindi katika mchezo wao wa jana wa kombe la Mapindizi dhidi ya Chipukizi uliochezwa Uwanja wa Amaan, uongozi wa Simba umewaomba radhi mashabiki kwa kushindwa kuwapa burudani kubwa.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema walikuwa na kikosi kizima ambacho waliamini kingefanikiwa kupata ushindi mnene badala yake wamepata ushindi mwembamba.
"Tuliwaahidi furaha na soka maridhawa watu wa Zanzibar na wale walioangalia kupitia Azam TV, bila shaka mmeridhika ila tunawaomba radhi kwa ushindi 'Mwembamba wa goli 4-1' tulioupata," alisema Manara.
Bao la kufutia machozi kwa Chipukizi lilifungwa na Evance Godwin ambaye alifunga bao maridadi sana akiwa kwenye eneo la 18 lililomshinda Ally Salim.
Ushindi mwembamba alioupata Sumba!
ReplyDeleteHakuna ushindi mwembamba
ReplyDeleteHakuna ushindi mwembamba mpaka Siku unalingana point na mwenzako....anasonga mbele au kuchukua kombe sababu ya magoli
ReplyDeleteLicha yakuwa Chipukizi ni timu dhaifu kulinganisha na Simba lakini ni thubutu kusema Simba ni timu iliyokusanya wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu hatarii. Waswahili wanasema usipokuwa na tahadhari na uvumilivu uliopitiliza kiwango basi uwezekano wa kula mbovu ni mkubwa. Lakini huu ustahamilivu wa ndani ya Simba kwa pande zote mbili. Kwa wachezaji wanaokosa kupangwa kikosi cha kwamza lakini wakaendelea kuwa wastahamilivu na kujituma kwenye mazoezi. Na kwa upande wa uongozi ambao wamewasajili wachezaji hao kwa gharama na kuendelea kuwapatia stahiki zao zote hata kama hawana mchango unaostahili kwenye timu kama ilivyotarajiwa lakini kiukweli wachezaji wengi wa reserve wa Simba wapo vizuri sana hivi sasa katika viwango vya kuvutia mno kazi ni kwa kocha mwenyewe kuwa na maamuzi sahihi katika kuwatumia. Haruna Niyozima amerudi kwenye kiwango chake au pengine yupo vizuri zaidi. Winga teleza Nicholasi Gayani yupo vizuri sana na nadhani viongozi wa Simba wasisahau kwa kijana alishawahi kuwa miongoni mwa wafungaji bora kule Ghana na hivi sasa anaonekana kuwa na hali ya kujiamini zaidi anapokaribia lango la wapinzani.kijana Rashid Juma yupo vizuri ni kipaji maridhawa. Saidi Ndemla yupo tayari kabisa kuingia vitani. Hata Mlipili ameonekana kuimarika. kwa kiasi fulani vijana hawa wakiendelea kuwa pamoja pale Simba basi huko twendako Simba haitashikika. La msingi ni kwa wachezaji wenyewe kutobweteka na mafanikio haya kiduchu bali waendelee kupambana kwani safari bado ni ndefu ya kuyafikia mafanikio halisi ila wachezaji mabadiliko yanaonekana hongereni sana Simba kwa kuonesha hali ya kustahimiliana.
ReplyDeleteSimba haina timu B, ina kitu kinaitwa super sub
ReplyDeleteKuna timu ya vijana ya simba. Hii sio timu B. Wale wengine ndio wana timu B, yaani kama lakwanza A,Lakwanza B.wote wapo lakwanza
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDelete