January 8, 2019


KIKOSI cha Simba kimefanikiwa kutinga kishujaa hatua ya nusu fainali ya kombe la Mapinduzi kwa kuweka rekodi ya kipekee baada ya kucheza michezo mitatu ya Kundi A.

Simba wanafanikiwa kuvuna pointi tisa zote baada ya kufanikiwa kushinda michezo yao ambayo wamecheza ya kombe la Mapinduzi.

Simba walianza na ushindi mbele ya Chipukizi kwa kushinda mabao 4-1 kisha wakawashushia kipigo cha bao 1-0 KMKM na leo wamefanya hivyo kwa Mlandege kwa kufunga bao 1-0.

Kwenye kundi A ambalo wapo Simba wanaongoza wakifuatiwa na KMKM, Mlandege kwa matokeo hayo wanayaaga mashindano, huku lile kundi B ni Azam FC na Malindi zinafanikiwa kuvuka hatua ya nusu Fainali na Yanga wakicheza kesho mchezo wa kukamilisha ratiba dhidi ya Jamhuri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic