January 11, 2019


Droo ya raundi ya nne na tano ya Kombe la Azam Federation Cup imechezeshwa katika makao makuu ya Azam na kushuhudia vigogo Yanga na Azam wakiendeleza bahati ya kucheza nyumbani.

Ratiba inaonesha Yanga watawakaribisha Biashara united kutoka mkoani mara huku azam wakicheza dhidi ya Pamba ya shinyanga.

Draw hiyo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiewemo wawakilish wa vilabu mbalimbali pamoja na waandishi wa habari, baadhi ya wawakilishi wa timu hizo  walikuwa na haya ya kusema baada ya draw hiyo kumalizika.

Mechi za raundi ya nne ya michuano hiyo zinatarajiwa kupigwa kati ya tarehe 25- 28 January huku round ya 16 bora ikipigwa kati ya february 21 – 25 mwaka huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic