UONGOZI wa Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC umesema kuwa meneja wa mchezaji wao Yahya Zayd amefuata taratibu zote za kumhamisha mshambuliaji huyo ambaye amekwenda kujiunga na timu ya Ismalia ya Misri.
Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema Zayd amekwenda jana nchini Misri atajiunga na klabu hiyo baada ya kukamilisha utaratibu wa kufanya vipimo vya afya ili aanze kutumikia majukumu yake mapya akiwa nje ya Azam FC.
"Meneja wa Zayd amefuata taratibu zote nasi tumebariki hasa kutokana na kutambua umuhimu wa mchezaji kucheza nje ya nchi hali itakayomfanya kuwa bora zaidi.
"Kuhusu suala la mkataba wake atasaini miaka mingapi, dau tutakalopata baada ya kumuuza tutaweka wazi kwani kwa sasa mchezaji yupo kukamilisha hatua za mwisho, kikubwa ni kwamba haendi kufanya majaribio ama kwenda kwa mkopo ameuzwa," alisema Maganga.
Zayd anakuwa mchezaji wa pili kucheza nchini Misri akitokea Azam FC baada ya Himid Mau ambaye ni nahodha msaidizi wa timu ya Taifa ambaye anaitumikia timu ya Petrojet.
0 COMMENTS:
Post a Comment