MENEJA wa mshambuliaji anayekipiga katika kikosi cha Mbeya City Eliud Ambokile amfunguka madili ambayo ana mpango ya kumuuza mchezaji wake huyo kwenye timu nyingine tofauti na Simba na Yanga.
Meneja amesema kuwa wachezaji wengi ndoto zao ni kucheza vilabu vikubwa hapa nchini lakini yeye kama malengo yake mchezaji asiishie hapa.
aombe sana Mungu Mbeya city ichukue ubingwa ili Ambokile aweze kuuzika vinginevyo ampeleke Kenya, Uganda au Afrika kusini ili aonekane bidhaaa iliyofichwa soko lake ni gumu sana. Ama vinginevyo meneja huyo anahitaji maslahi ambayo hayajulikani kwake ama mchezaji husika kama sio kudanganyana
ReplyDeleteHizo ni ndoto. Simjui watu wengine wanapata vigugumizi gani kusema ukweli kwamba Tanzania yetu wababe wa mpira kwa miaka mingi ni Yanga na Simba. Mchezaji kujulikana kwingineko na kupata soko zuri ni rahisi zaidi akitokea Simba au Yanga kuliko kumtangaza akiwa Mbeya au Lindi. Huo ndio ukweli. Tuache kudharau timu zetu wenyewe zinazotuletea sifa na heshima kwa nchi yetu. Baada ya kuona Salamba na Mohamed Rashid walivyokuwa wanawika mikoani na yaliyodhihirika walipokwenda Simba, hivi una uhakika gani kwa Ambokile atatakiwa na Yanga au Simba kwa mpira gani hasa? Wangu mimi ingetokea vilabu hivyo Simba, Yanga, Azam vikamtaka, ni afadhali akubali kwenda fasta ili akaonekane kule baadae atapata ofa ya maana kutokea hapo kwenda vilabu vikubwa vya nje.
ReplyDelete