VITA YASIMAMISHA MAZOEZI SIMBA
Simba juzi Jumatatu walishindwa kuanza mazoezi yao takribani dakika 20 huku wakitumia muda huo kwa ajili ya kuzungumzia mambo ya timu hiyo hasa mechi yao iliyopita dhidi ya AS Vita iliyopigwa nchini DR Congo.
Simba walitumia muda huo kwa ajili ya kuzungumza juu ya mambo ya kikosi hicho kuhusiana na mechi hiyo iliyopita sambamba na kupeana maelekezo mbalimbali.
Kikosi hicho kilizungumza masuala hayo wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika juzi Jumatatu katika Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar.
Katika kikao hicho, kocha Patrick Aussems ndiye aliyekuwa anazungumza kwa muda mrefu sambamba nyota wa timu hiyo, Emmanuel Okwi.
Aussems alianza kuzungumza na nyota wake ambao walisimama kwa duara saa 9:53 alasiri akiwapa maneno mbalimbali sambamba na Okwi ambaye alikuwa anakazia na mazungumzo hayo kumalizika saa 10:11 alasiri.
Championi Jumatano ambalo lilikuwepo katika mazoezi hayo, lilishuhudia mchezo mzima wa tukio hilo mwanzo mpaka mwisho. Simba Jumamosi iliyopita walikubali kichapo cha mabao 5-0 mbele ya AS Vita ukiwa mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa kwa timu hiyo kucheza.
Simba wanashika nafasi ya tatu katika kundi lao wakiwa na pointi tatu, ambalo linaongozwa na Al Ahly wenyewe pointi nne.
CHANZO: CHAMPIONI
Upuuzi..eti mazoezi yamesimamishwa dakika 20! Tafuteni cha kuandika..Halafu saleh jembe sio kila takataka wanayoandika champion na nyie mnakopy..Wandishi wenu wakiandika habari hawaweki majina!lakini upuuzi wa champion mnaweka chanzo ni nani
ReplyDelete