January 23, 2019


UONGOZI wa Simba umesema kuwa utatumia mchezo wao wa leo wa SportPesa utakaochezwa Uwanja wa Taifa kupooza machungu ya mashabiki baada ya kupigwa mabao 5-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa nchini Congo.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema anatambua ugumu wa mashindano pamoja na uimara wa wapinzani wao AFC Leopards ila watatumia uzoefu wao kupata matokeo kwenye mchezo wao wa leo.

"Tunajua mashabiki wana maumivu hata sisi pia tunamaumivu ya kupoteza mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa, tutatumia mchezo huu kuonyesha kwamba tunaweza na tutafanya kazi kubwa kutafuta ushindi.

"Wapinzani wetu nao wana jina la mnyama mkali hivyo leo itakuwa vita nasi pia tutapambana kutafuta matokeo mashabiki wajitokeze kuona ubora wetu," alisema Manara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic