January 16, 2019


MABINGWA wa kihistoria, Yanga wamekosa mfano msimu huu kutokana na kuwa na mwendo mkali kwenye Ligi Kuu Bara tofauti na msimu uliopita wa mwaka 2017/18.

Yanga kwa msimu uliopita baada ya kucheza michezo 19 walikuwa wamefanikiwa kushinda michezo 10 tofauti na msimu huu ambao wameonyesha kuwa wana moto baada ya kushinda michezo 17.

Kwa upande wa sare msimu uliopita Yanga walikuwa na sare  nane tofauti na msimu huu  mpaka sasa wamepata sare mbili pekee Ligi Kuu Bara.

Kwa upande wa kupoteza msimu uliopita walikuwa wamepoteza mchezo mmoja baada ya kukubali kufungwa bao 2-0 dhidi ya Mbao ila msimu huu wamekuwa tofauti kwa kutoruhusu kufungwa hata mchezo mmoja.

Wamekuwa mbali pia hata kwa upande wa mabao ya kufunga ambapo msimu uliopita walifunga jumla ya mabao 30 ila kwa sasa wana jumla ya mabao 38inaamaanisha kwamba safu ya ushambuliaji imekuwa na makali kwenye ligi na kwa upande wa nafasi walikuwa wa pili baada ya kukusanya pointi 38 na msimu huu wanaongoza Ligi wakiwa na pointi 53

Tofauti kubwa ni kwa upande wa mabao ya kufungwa ambapo msimu uliopita walifungwa mabao 9 pekee ila msimu huu wamekuwa na beki nyanya kwani wameruhusu kufungwa jumla ya mabao 12 kwenye Ligi Kuu Bara. 

3 COMMENTS:

  1. Lakn Simba Ni champion 2019 hlo niwakae moyon

    ReplyDelete
  2. We vituko soka halichezewi mdomoni ni uwanjani...subiri ligi iendelee...

    ReplyDelete
  3. Kwa Kotei nakubaliana na Mwandishi 100%

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic