January 16, 2019


Mwaka 1989 Simba Sports ilimsajili mchezaji toka timu ya mtaani tu huyu si mwingine ni Iddi Selemani Kibode wengine walipenda kumuita MaYOR na wengine hasa wachezaji wenzie walipenda kumuita nyigu.

Mwenyeji wa matombo mkoani morogoro mji kasoro bahari, huyu ni ndugu na mfungaji bora wa ligi kuu tanzania bara mwaka 1989 Madaraka Selemani Kibode ambaye aling'ara akiwa na Simba na timu ya taifa (kwa wale waliokuwa hajui nani alikuwa mfungaji bora ligi kuu tanzania bara mwaka huo chukueni hiyo ni madaraka akiwa anaichezea Majimaji ya Songea).

Huyu alikuwa kiungo mkabaji pia alimudu kucheza kama beki wa kati "libero" mashabiki wengi hawakujua Simba wamemtoa wapi, nyigu aliitwa hivyo kutokana na staili yake ya "kuwatengeneza" kuwafinya wachezaji wa timu pinzani waliokuwa wasumbufu kwa timu yake hasa wanapokaribia eneo la hatari na ni mara chache sana kuonwa na refa.

Nyigu hakuwa na vitu vingi kama kupiga chenga za maudhi au kupiga kanzu hapana yeye kazi yake kubwa ilikuwa kutibua mipango ya timu pinzani tu na kuhakikisha safu ya ulinzi inakuwa salama wakati wote wa mchezo.

Simba ilikuwa na viungo mafundi wengi kama adolph kondo, Method Mogella, amadhani lenny, hussein marsha na hamza maneno kwa nyakati tofauti ila hawa wote wamecheza na nyigu lakini mechi muhimu zote hakuwahi kuachwa nje hasa Simba ilipocheza na yanga kama huamini unachokisoma watafute makocha Abdallah Kibaden au Dragan Popadic aliofanya nao kazi Simba uwaulize watakuthibitishia hili.

Kwenye kikosi cha sasa cha Simba skuna mtu anaitwa James Agyekum Kotei raia wa Ghana, huyu ni mmoja kati ya wachezaji muhimu mno lakini haimbwi wala kupambwa sana na vyombo vya habari ama mashabiki kwa kuwa tu hapigi chenga za maudhi, hatoi pasi za visigino wala hapigi kanzu lakini cha ajabu makocha wote wanaofika simba lazima wampe nafasi kikosi cha kwanza unajua kwa nini?

Kuanzia kwa Joseph Omog, Masoud Djuma, Pierre Lechantre mpaka Kocha wa sasa, Mbelgiji, Patrick Aussems, bado umuhimu wa kotei Simba hujawahi kukosekana, anajua kuilinda safu yake ya ulinzi vizuri, anamudu kuwatengeneza "kuwafinya" wachezaji wa timu pinzani wanaonekana kuwa na madhara kwa timu yake na hajawahi kupewa kadi nyekundu toka atue Simba, anafanya hivyo vyote kwa umakini wa hali ya juu sana

Ukiwauliza wapenzi wa soka kuhusu viungo bora simba wanaweza kukutajia mpaka majina matano ila miongoni mwao jina la Kotei halitokuwepo amini usiamini lakini cha ajabu hakosekani kwenye mechi zote muhimu za timu hiyo, Kotei kama ilivyokuwa kwa Iddi Selemani yeye pia ni kiungo mkabaji mwenye uwezo mkubwa wa kucheza beki wa kati pale inapotokea dharura.

Mfano mzuri ilikuwa Februari 26 mwaka 2017 kwenye mchezo wa watani wa jadi Simba vs Yanga baada ya Javiex Basela Bukungu kutolewa nje kwa kadi nyekundu jukumu la kwenda kucheza beki wa kati ili kusaidiana na Abdi Banda alipewa Kotei na alicheza vizuri mno mpaka Simba wakamudu kusawazisha bao na kuongeza bao la ushindi

Huyo ndiyo James Agyekum Kotei gurudumu lisilo na pacha linaloitembeza simba kimya kimya.

Na Abubakar Mohamed Mbwana

1 COMMENTS:

  1. Hiki kigingi kwa asiye jua mpira anaweza kuona ni wa kawaida, ila unaweza kuona kuwa ni defending midfielder wa ukweli, hata likitokea kosa likafungwa ujue aidha kamtegea Mkude akabe na Mkude akashindwa au makosa ya kibinadamu, lakini ni kweli anajua kukata umeme kwa kukaa njia na anjituma sana sana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic