January 9, 2019


TIMU ya Yanga, leo Jumatano itacheza mechi ya mwisho ya Kombe la Mapinduzi mwaka huu dhidi ya Jamhuri ya Pemba, kisha itapanda boti na kurejea Dar kutokana na kutokuwa na chake kwenye michuano hiyo.

Yanga katika michuano hiyo imeshindwa kufanya vizuri kutokana na kucheza mechi tatu na kujikusanyia pointi tatu baada ya kushinda moja na kufungwa mbili.

Yanga na Jamhuri zitacheza mechi hiyo ya Kundi B kwenye Uwanja wa Amaan kuanzia saa kumi jioni.

Katika kundi hilo, Azam inaongoza ikiwa na pointi saba sawa na Malindi ambazo zote zimefuzu nusu fainali. Jamhuri ina pointi nne, Yanga (3) na KVZ inaburuza mkia na pointi moja.

Michuano hiyo ambayo ilianza Januari Mosi, mwaka huu, inazishirikisha timu tisa, tatu za Tanzania Bara na sita za Zanzibar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic