BONDIA Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’, amefunguka kwamba kama bondia Hassan Mwakinyo atataka kupambana naye basi anamsubiri kwa sharti moja la bondia huyo apandishe kilo zake.
Mbabe amesema kwamba kwa sasa hawezi kupambana na Mwakinyo kwa sababu bondia huyo ana kilo ndogo tofauti na yeye ambaye amemzidi kwenye suala la uzito.
“Mashabiki wanataka nipambane na Mwakinyo ila haitakuwa kwa sababu mimi ninacheza Middle Weight kilo 76 hadi 79 ila yeye anacheza 69 hadi 72, kama atataka basi aongeze kilo hadi 74 hapo, kisha tutapambana,” alisema Mbabe.
unachelewa kuweka habari mwamba
ReplyDelete