January 9, 2019


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ametamba kwamba kwa sasa hana wasiwasi na mechi yao dhidi ya Simba kutokana na kuimarika kwa kikosi chake tofauti na walivyokutana kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu.

Katika mchezo wa kwanza ambao uliwakutanisha Simba na Yanga, Septemba 30, mwaka jana, Zahera alitumia mfumo wa kujilinda zaidi kutokana na kikosi chake kuwa kidogo lakini mchezo huo ukamalizika kwa suluhu. Kwenye mzunguko wa pili, Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana Februari, mwaka huu.

Kocha huyo mwenye uraia wa DR Congo na Ufaransa, alisema hana hofu ya kucheza na Simba kwa sababu amefanya usajili wa kuiongezea nguvu timu yake wa Haruna Moshi ‘Boban’ huku Mohammed Issa ‘Banka’ naye atakuwa ameshaanza kuitumikia timu hiyo.

“Wakati wa mzunguko wa kwanza nilikuwa naogopa kucheza na Simba ndiyo maana tulipokutana nao tulijilinda sana, kwa sababu wao walikuwa na kikosi kikubwa zaidi kuliko kile cha kwetu na walikuwa na wachezaji wazuri.

“Lakini kwa sasa sina hofu tena ya kucheza nao hata kidogo kwa sababu tumeboresha timu na tumefanya usajili wa Boban ambaye amekuja kutusaidia na kuongeza nguvu.

“Lakini pia kwa sasa tuna kikosi kikubwa na jambo zuri kabla ya kukutana nao, pia Banka naye atakuwa tayari yupo kwenye timu yetu, utaona ni kikosi gani ambacho nitakuwa nacho wakati ambao tutacheza na Simba katika mzunguko wa pili,” alisema kocha huyo.

1 COMMENTS:

  1. acha uongo. umetunga hii story upate ratings. Tumeshakusoma wewe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic