February 25, 2019


MARA baada ya Azam kumvunjia mkataba kocha wake Mholanzi, Hans van Der Pluijm mapema juzi, imebainika kwamba uongozi huo tayari umepokea zaidi ya wasifu wa makocha 10 ambao wameomba kibarua kikosini hapo.

Azam FC, juzi Jumamosi walitangaza kuachana na Pluijm pamoja na msaidizi wake, Juma Mwambusi ikiwa ni baada ya timu hiyo inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu, kuwa na matokeo mabaya kwenye mechi zake tano zilizopita ikiwemo ya Simba. Lakini ndani ya siku moja tu, tayari wameshapokea wasifu ‘CV’ za makocha 10.

Makamu Mwenyekiti wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’, amesema mara baada ya wao kuachana na Pluijm, tayari hadi jana walikuwa wamepokea ‘CV’ za makocha wapatao 10 ambao wanataka mikoba ya Mholanzi huyo ingawa kwa sasa timu ipo chini ya makocha wa muda, Meja Abdul Mingange na Idd Cheche kutoka timu za vijana za Azam. 

“Idadi inaongezeka tu kila mara lakini tukishakaa viongozi ndiyo tutaamua tufanye nini,” alisema Popat.

2 COMMENTS:

  1. Ilisemekana kuwa Zahera nae angeingia katika hicho kinyanganyiro

    ReplyDelete
  2. Azam FC sometyms patient pays you guys u too first in making decisions which will cost the team....I watched ua game against simba FC Boccos goal he was alone n nobody hanged wth him free header now what does coach do..nwe wish u luck.. inshallah.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic