KABWILI APELEKA MACHUNGU HAYA SIMBA
LICHA ya baadhi ya mashabiki wa Yanga kutokuwa na imani na kipa wao Ramadhani Kabwili, mlinda mlango huyo amesisitiza kwamba yeye ndiye atakayewapa ubingwa.
Kabwili amejipatia umaarufu na nafasi ya kudakia katika kikosi cha Yanga baada ya kuondoka kwa kipa namba moja, Beno Kakolanya ambaye ameondolewa katika kikosi hicho baada ya kuigomea timu hiyo kwa kudai maslahi.
Kabwili ameanza kuidakia timu hiyo tangu mzunguko wa kwanza wa ligi kuu mara baada ya kuondoka Beno huku akisaidiana na Klaus Kindoki ambaye amekuwa hapewi nafasi sana kutokana na kiwango chake kutoaminika.
“Nitajituma kwa moyo wote kuhakikisha timu yangu ya Yanga inatwaa ubingwa msimu huu kwa kuhakikisha naidakia ipasavyo.
“Kwa upande wangu sina wasi na nafasi yangu hii niliyoipata ya kudaka kama kipa wa kutegemewa kwa sasa na kikubwa kwangu ni kuona naendelea kujituma ili kiwango changu kiendelee kuwa juu,” alisema Kabwili.
Kauli hiyo ya Kabwili inakuwa kama inawaumiza mashabiki wa Simba kutokana na wao kuwa kwenye mbio za kuutetea baada ya kuchukua msimu uliopita.








Mbona hayo maneno tu..hata kwenye kanga yapo..Simba aki clear viporo vyote anaongoza kwa point 5 sasa atasemaje ataidakia team yake mpaka ichukue ubingwa wa ligi labda ligi ijayo kwa maana hii ndo ishakula kwao, na pia ligi ijayo usajili ukiwa hivi watabakia kugonga story... ingekuwa labda kabwili anaweza kudaka viporo vya Simba labda mashabiki wangeumia...sema uanachotakiwa kusema na wewe mwandishi ukakiandika ni KABWILI AMESEMA ATAIDAKIA TEAM YAKE KUAKIKISHA ANAKUWA KIPA NAMBA MOJA....asiongee habari za ubingwa kama wanataka ubingwa wafanye uchaguzi kwanza.
ReplyDeleteToka lini Kabwili akachezea Simba?
ReplyDeleteSimba wakishinda mechi zao watakuwa mabingwa. Na huo ndio ukweli.
Kuwa na viporo haina maana ndio uhakika wa ushindi...
ReplyDelete