February 9, 2019


Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Wallace Karia, amesema hajui kama CHADEMA wamepeleka barua FIFA baada ya kumtaja Tundu Lissu katika Mkutano Mkuu wa TFF uliofanyika jijini Arusha siku chache zilizopita, imeelezwa.

Taarifa inasema Rais huyo ameeleza kutokuwa na taarifa yoyote juu ya barua hiyo na akisema hajajua haswa kilichoandikwa nini ndani yake.

Katika Mkutano uliofanyika jijini Arusha, Karia aliwakemea baadhi ya viongozi ambao wanamuunga mkono Wambura pia akiwataja wale wenye tabia za ajabu kwa kusema 'Matundu Lissu' kitu ambacho CHADEMA kiliwakera.

Kutokana na kauli hiyo, CHADEMA iliamua kukaa chini na kuandika barua kutoka Idara ya Habari na Mawasiliano iliyo chini ya Tumaini Makene na kupelekwa FIFA huku nakala yake ikipitia Shirikisho la Soka Africa (CAF).

Baada ya CHADEMA kufanya maamuzi hayo, Karia aliamua kufunguka kwa kueleza hajui chochote na wala hawezi kuzungumzia suala lolote juu ya wao kwenda FIFA huku akieleza ufafanuzi alioutoa siku baada ya mkutano unatosha.

7 COMMENTS:

  1. Chadema ubaguzi ndio wenu utamwitaje mtanzania halisi msomali? Chama cha matabaka na ukanda. Kama Karia kenge? Lisu atakuwa nani Ngedere?

    ReplyDelete
  2. Asubuhi Nilisema Karia Katuletea Siasa Mpirani Jamani Karia Kakosea Tena "Sana" Asichukulie Poa

    ReplyDelete
  3. Katika mahojiano yake yote Tundu Lisu aliyofanya katika dhiara yake ya kuipaka mavi Tanzania barani ulaya na Marekani karibu kila mtu aliefanya nae mahojiano,Lisu aliulizwa kama kuna jambo lolote ameliona zuri serikali ya awamu ya tano imelifanya kwa manufaa ya nchi? Jibu la Lisu ni hapana hakuna hata moja zuri serikali ya awamu ya tano ililofanya isipokuwa ni kuerejesha nchi myuma. Yaani amekataa katukatu kuwa kuna chochote cha maana kilichofanywa na serikali ya Magufuli. Lisu alipoulizwa na mtangazaji kule Washington DC kwamba watanzania wanalalamika kuwa anawachafulia taifa lao. Yeye akajibu watu wanashindwa kuelewa kati ya serikali na Taifa. Yaani sawa na mtu aliekiri kumchokonoa rubani angani wakati ndege ikiwa safarini na abiria wake wakiwa na matumaini tele ya kufikishwa salama wanapoelekea kwenda,alafu anatokea muendawazimu anasema abiria msiwe na wasiwasi hata kidoga na ndege yenu kwani rubani na ndege ni vitu viwili tofauti kabisa mimi ninachokifanya ni kumtia pirika rubani mpaka kieleweke ndege yenu itakuwa salama? Hizo ndizo akili za Tundu Lisu na mabumbula mitandaoni yakipiga makofi. Kama wapo wanaokubaliana na harakati za kifisadi za Lisu zidi ya nchi yetu basi wajue wana matatizo na kamwe hawatashinda. Yeye mwenyewe Lisu anajikweza kujivimbisha kichwa kuwa ni mpinzani wa Magufuli? Ooo Lord. Lisu hata akisimamishwa na khaji Manara basi Manara ataibuka kidedea,kubwa zaidi watu wake wa karibu Lisu wamfahamishe juu ya kuyaheshimu mamlaka kwani anakwenda kimyume na mafundisho ya Dini zote ujumbe kuoka kwa Mwenyezi Mungu kwamba waja wake wana wajibu wa kutii na kuheshiimu mamlaka za nchi zao au wakaidi kuzitii na kuishi maisha ya mateso. Walibya waliipuuza maagizo hayo ya Mwenyezi Mungu na kilichowapata haina haja ya kurejea kusimulia tena. Fikiria,Mmarekani,Muengere-za Mfaransa,Mjerumani, na vibaraka vyao wengine wameshindwa kuiunganisha Libya na kurejesha hali ya amani angalau kwa mwezi mmoja. Lakini Gadafi mmoja peke yake aliweza kuituliza Libya kwa miaka. Lakini kiuhalisia Gadaf hakuweza kwa nguvu zake ila Mungu alipanga na kwa walibya kukiuka Maagizo ya Mwenyezi Mungu sasa wanateseka.Wewe unafikiri Asadi wa Siria ana nguvu gani yakubakia madarakani mpaka leo? Kiuhalisia sio nguvu zake ila Mungu amepanga awepo pale na kwa baadhi ya wananchi wake kupuuza kufuata maagizo ya Mwenyezi Mungu ya kutii mamlaka wakateseka na wanaendelea kuteseka kwa wanaoendelea kukaidi. Huo ndio ukweli,hakuna Marekani,hakuna cha umoja wa ulaya. Lisu,chadema na wale wote wanaodhamiria kutotii Mamlaka ya nchi wanapingana na Maagizo ya Mwenyezi Mungu ya kutii mamlaka ya nchi kwa hivyo basi wameamua kujichagulia maisha ya mateso ya kujitakia kwani maagizo ya Mwenyezi Mungu kamwe hayapindiki husimama daima na ukweli wake mtu atake asitake.

    ReplyDelete
  4. Imeandikwa mwenye haki akitawala watu huwa na furaha kwa hiyo basi kama watu wahafurahi ,................???????

    ReplyDelete
  5. Sheitani au Iblisi ndie muanzilishi wa ukaidi. Iblisi hakuwa na dhiki wakati anambishia Mwenyezi Mungu alipowaamrisha malaika kuonesha utukufu kwa adamu alipomuumba. Hiyo inamaanisha yakwamba ukaidi kwa kiumbe ni kibri na hahihalisi kama mtu anafuraha au la ni ushetani tu. Walibya usafiri wa ndani ulikuwa bure,huduma za Simu bure,Masomo kwa wanafunzi ndani na nje ya nchi bure,wanandoa wapya makazi bure,Mtoto akizaliwa tayari ana akaunti ya dollar 5000$,nakadhika nakadhalika. Sasa utaona kama wenye akili zao wakiyaacha mawazo ya kishatani yachukue nafasi kwenye jamii basi ndio yale yaliyotokea Libya.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic