February 3, 2019


Kufuatia kichapo cha mabao 5-0 ilichokipata Simba dhidi ya Al Ahly katika Ligi ya Mabingwa Afrika, mashabiki wa Simba wametoa maoni yao.

Mashabiki na wanachama kadhaa wameutaka uongozi kuchukulia maanani uzito na ukubwa mashindano hayo kwani imesababisha matokeo yawe mabaya.

Wameeleza kuanzia katika ngazi ya usajili Simba ya sasa haina haja ya kusajili wachezaji wa majaribio haswa katika mashindano makubwa kama haya.

Hatua hiyo imekuja kutokana na Simba kuleta wachezaji wa majaribio hivi karibuni jambo ambalo wengi wamekuwa wakilipinga.

Wameeleza ili Simba iweze kufanya vema kwenye hatua kama hii ya makundi ni vema kusajili wachezaji wenye uwezo na si majaribio jambo ambalo halitaifisha popote timu.

11 COMMENTS:

  1. Uongozi uliokuwepo madarakani bora kusingefanyika uchaguzi.Inaonekana kukosekana watu kama Kassim Dewji, zakaria Hanspop nakadhalika kumeiingiza simba kwenye Chaka wasijue wapi wanakoelekea. Viongozi gani wasiosikiliza ushauri?

    ReplyDelete
  2. Simba walikuwa na uwezo kumpiga tano bila js Saoura kama wangekuwa makini ila tunarudi pale pale wachezaji wanakosa umakini.

    ReplyDelete
  3. Tusidanganyane, simba ni mbovu, kama mapinduz imepigwa, sport pesa imepigwa tena jana tungepigwa nane hizo tano za kipindi cha kwanza kwa al ahly ni chache, na walituonea huruma, kocha hafai wanasimba.

    ReplyDelete
  4. Nitaanza kuangalia mechi za simba hadi kocha atakapoondoka

    ReplyDelete
  5. Kiukweli inauma sana, naendelea kuwa mvumilivu mpira ndivyo ulivyo, karibuni Korogwe - Tanga.

    ReplyDelete
  6. Ni aibu kubwa sna tena haijawahi kutokea mechi mbili goli kumi tena tao tano kwa mfululizo pumbavuuuuuu

    ReplyDelete
  7. Hovyo kabisa kupita maelezo. Timu inakatisha tamaa kabisa.

    ReplyDelete
  8. Yaani ni hovyo kabisa kupita maelezo.

    ReplyDelete
  9. Kinachoua soka la Tanzania ni mwingiliano wa soka na siasa maana viongozi wote wanajihusisha ktk siasa badala ya kitengo husika, any way ilipofikia club km simba c ya kuchukua wachezaji wa majaribio kifupi simba haipo siliasi na hii ligi ila watu wako bize na upigaji pesa tu, then atakuja mtu analopoka na kututaka tutulie wakati cc tunaumia,

    ReplyDelete
  10. Toka nianze kuishabikia Simba Sports Club mwaka 1968 ikiitwa Sunderland na kupigwa goli 5-0 na Yanga...tokea mwaka huo sikumbuki kama Simba ilishapigwa goli 5-0.Kwa kweli siamini goli 10-0 ndani ya wiki mbili?
    Kwa nini kocha hataki msaidizi? Kwa nini mnatafuta wachezaji wa majaribio?Niko hapa Uarabuni na marafiki zangu wamisri wanasema kocha anapaswa kuwajibika pale atakapofika airport.Na viongozi angalieni makocha toka Serbia, Croatia, Romania na hata Uholanzi.Ni bora hata kumwomba kwa muda Popadic au Kibadeni.

    ReplyDelete
  11. Ujinga mtupu huu! Bado watatuletea habari za kuwa "malengo yetu na kocha ni kombe la ligi na kuingia hatua ya makundi". Utawasikia tu!!!, sasa kama ni hivyo c bora muitoe timu katika mashindano ya klabu bingwa! maana c tayari mmefanikiwa kuingia makundi!, sasa hii ni aibu gani inayoendelea! Na JS Soura wanatusubiri kwao, kule tunaenda kupigwa hata 7.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic