February 25, 2019




ACHANA na mabao 11 aliyonayo kwa sasa, mshambuliaji wa Simba mwenye mwili wa aina yake na spidi eneo la hatari, Meddie Kagere ona jinsi alivyolitafuta bao lake la 11 kwenye nyavu za Razack Abarola.

Kwenye mchezo wao juzi uwanja wa Mkapa dhidi ya Azam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1  Kagere alitafuta bao la tatu kwenye nyavu ili kuona mpira kwenye lango la Razack Abarola raia wa Ghana.

Bao hilo alifunga dakika ya 77 likianzia kwa Mzamiru Yassin kabla ya Clatous Chama kutoa pasi safi ambayo ilimkuta Kagere aliyeachia shuti likazuiwa na Yakubu Mohamed akalilazimisha likazama langoni aliamua kulifuata akiwa na wenzake Zana Coulibaly na Clatous Chama kuutafuta mpira.

Kagere amesema kuwa anaona fahari kuipa pointi tatu timu yake kwani hizo ni hesabu za kila mchezaji na alichokifuata kwenye lango la Abarola ilikuwa ni furaha kuzidi.

"Unajua mpira ni burudani na ubunifu, sasa baada ya kufunga lile bao sikujua kama mpira umerudi uwanjani ama umetoboa nyavu nikaanza kuufuata na wenzangu wakanifuata ikawa burudani tu, ila ninashuru kwa matokeo," alisema Kagere.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic