February 25, 2019



NAHODHA wa Simba, John Bocco ameweka rekodi ya aina yake katika michezo aliyopata nafasi ya kuifungia timu yake kwani mechi zote alizofunga Simba ilishinda mabao matatu.

Bocco ambaye msimu uliopita alitupia mabao 14 na msimu huu aliliambia SpotiXtra kuwa atafunga mabao mengi zaidi ya hayo alianza kwa kusuasua kutokana na kusumbuliwa na majeruhi na alifungulia bao lake la kwanza kwenye mchezo wake dhidi ya Mwadui.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mwadui Complex Bocco alifunga mabao mawili na bao la tatu likafungwa na Meddie Kagere na kufanya Simba ishinde mabao 3-1.

Pia katika mchezo wake dhidi ya Singida United, Bocco aliifungia timu yake na ilishinda mabao 3-0, pia kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Mwadui Bocco alifunga bao moja na kuiongoza Simba kushinda mabao 3-0.

Hakuishia hapo mchezo wake dhidi ya African Lyon alitupia mabao mawili na mchezo ulikamilika kwa mabao 3-0, juzi aliendeleza rekodi hiyo baada ya kuwatungua mabosi wake wa zamani Azam FC Simba ilishinda mabao 3-1, rekodi hii haijawekwa na nahodha yoyote bongo kwa sasa.

Bocco mpaka sasa ana mabao saba huku timu yake ikiwa imefunga mabao 38 ikiwa nafasi ya tatu na pointi 45, Azam wapo nafasi ya pili na pointi 50, wakiachwa nyuma na wapinzani wao Yanga ambao ni vinara wenye pointi 61.


2 COMMENTS:

  1. Yaliopita ya ushindi yamepita Wachezaji wa Simba wanatakiwa kuwaondelea hofu, wasi wasi na mashaka kwenye hizi mechi zao za mikoani kwani mara nyingi wamekuwa wakikubali kukamiwa na wachezaji wa vijitimu hata kulipwa mishahara hawalipwi labda ndio maana wachezaji wa hizi timu hujituma na kukamia zaidi mechi za Simba au Azam kwa juhudi zao binafsi ili kuvivuitia vilabu vikubwa kwa ajili ya kupata ajira bora zaidi na kwa kweli sio kitu kibaya hata kidogo bali ubaya upo kwa wachezaji kama wa Simba kukubali kwenda kufungwa au kupata matokeo ya sare na timu kama lipuli. Kwa kiasi fulani huwa haingii akilini hata kama lipuli wanacheza yumbani kwao.Hata kama lipuli wana kocha anaeufahamu udhaifu na uimara wa Simba upo wapi na sio kama naibeza lipuli hapana ila ukiangalia kwa macho tu wachezaji gani kati ya lipuli na Simba wanaorahishiwa kufanya kazi yao bila ya bugudha,nazungumzia vifaa ,maslahi,walimu bora nakadhalika nakadhalika. Na sio kama Simba isifungwe na lipuli la hasha hapana bali imeshakuwa mazoea sasa kwa Simba kuchemsha kwa lipuli. Kwa kiasi kikubwa kila timu inayocheza na Simba watakimbilia kuidhibiti Simba kunako eneo la kiungo sasa kuna vitu vingine mchezaji wa mpira sio kila kitu kuambiwa na kocha kila siku nini cha kufanya ni ufahamu na juhudi binafsi katika kuipigania timu kupata ushindi. Na nnavyoamini mimi Simba ni kwao zaidi Iringa kuliko hata lipuli fc. Mechi ya mzunguko wa mwanzo Simba walishindwa kuwafunga lipuli fc pale Dar kisingizio kikawa uwanja mdogo. Mara hii labda wakishindwa Simba kupata ushindi na lipuli wanaweza kusinguzia mechi ilikuwa ya ugenini? Lakini kama Simba atashindwa kuifunga lipuli ugenini,vipi Js Saoura ndani ya Algeira? Kweli Simba imebadilika kiuchezaji lakini bado Wachezaji wanatakiwa kuonesha utofauti zaidi wa ubora kati yao na wachezaji wa ligi ya ndani na kama kukamiwa basi na wao wanapaswa kuonesha wao ni level ya juu zidi na ndio maana wanaiwakilisha nchi kimataifa.

    ReplyDelete
  2. Shime jamani kazi kesho muimalize mapema nasi tupate kutanafasi manaake huyu Matola ana anajitia tamaa nyingi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic